Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Marko 11:27-33

Marko 11:27-33 NENO

Wakafika tena Yerusalemu, na Isa alipokuwa akitembea Hekaluni, viongozi wa makuhani, walimu wa Torati pamoja na wazee wa watu wakamjia. Wakamuuliza, “Unafanya mambo haya kwa mamlaka gani? Na ni nani aliyekupa mamlaka ya kufanya hayo?” Isa akawajibu, “Nitawauliza swali moja. Nijibuni, nami nitawaambia ni kwa mamlaka gani ninafanya mambo haya. Je, ubatizo wa Yahya ulitoka mbinguni au kwa wanadamu? Niambieni!” Wakahojiana wao kwa wao na kusema, “Tukisema, ‘Ulitoka mbinguni,’ atatuuliza, ‘Mbona hamkumwamini?’ Lakini tukisema, ‘Ulitoka kwa wanadamu’ ” (waliwaogopa watu, kwa sababu kila mtu aliamini kwamba Yahya alikuwa nabii wa kweli); kwa hiyo wakamjibu Isa, “Hatujui.” Naye Isa akawaambia, “Wala mimi sitawaambia ni kwa mamlaka gani ninatenda mambo haya.”