Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hesabu Utangulizi

Utangulizi
Kitabu cha Hesabu kimepewa jina hili kutokana na matukio mawili ya kuwahesabu wana wa Israeli: La kwanza huko Sinai katika mwaka wa pili baada ya kutoka Misri (Hes 1), na la pili huko Yordani katika mwaka wa arobaini (Hes 26). Jina la kitabu hiki kwa Kiebrania ni “Bemidbar,” ambalo maana yake ni “Huko jangwani,” jina linaloelekea kueleza zaidi yale yaliyomo.
Kitabu hiki kinatoa maelezo ya safari ya Waisraeli ya miaka 38 wakati walikuwa wanatangatanga jangwani baada ya kuanzishwa kwa Agano la Mungu katika Mlima Sinai. Kitabu cha Hesabu kinagusia safari ya Waisraeli kutoka Mlima Sinai hadi nchi tambarare ya Moabu katika mpaka wa Kanaani. Kitabu hiki kinaelezea vile Waisraeli walivyonungʼunika na kumwasi Mungu, na hukumu iliyofuata baadaye. Watu wazima waliotoka Misri walikosa nafasi ya kuingia katika Nchi ya Ahadi, isipokuwa watoto wao.
Mwandishi
Mose.
Kusudi
Kuelezea jinsi Waisraeli walivyojitayarisha kuingia katika Nchi ya Ahadi, na walivyoasi na kuhukumiwa.
Mahali
Kitabu hiki kiliandikwa wakati Waisraeli walikuwa wanatangatanga jangwani, mahali fulani katika Ghuba ya Sinai.
Tarehe
Kati ya 1450–1410 K.K.
Wahusika Wakuu
Mose, Aroni, Miriamu, Yoshua, Kalebu, Eleazari, Kora, Balaamu na Balaki.
Wazo Kuu
Kitabu hiki kinaeleza juu ya utunzaji na uongozi wa Mungu, uvumilivu wake, na uasi wa watu wa Mungu na matokeo yake. Jambo moja lililokuwa dhahiri na ambalo limerudiwa mara kwa mara katika kitabu chote ni jinsi mkono wa Mungu ulivyokuwa pamoja na wana wa Israeli saa zote ili kuwahudumia na kuwapa mahitaji yao.
Mambo Muhimu
Kuhesabiwa kwa Waisraeli, uasi dhidi ya Mungu, na hukumu ya Waisraeli ya kutangatanga jangwani.
Mgawanyo
Maelezo ya Hema la Kukutania, na kuendelea na safari (1:1–10:10)
Kutoka Sinai hadi nchi tambarare ya Moabu (10:11–21:35)
Balaamu, Balaki na Israeli (22:1–25:18)
Maelekezo juu ya kuishinda na kuitwaa nchi ya Kanaani (26:1–36:13).

Iliyochaguliwa sasa

Hesabu Utangulizi: NEN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia