Wafilipi 1:1-8
Wafilipi 1:1-8 NENO
Paulo na Timotheo, watumishi wa Al-Masihi Isa. Kwa watakatifu wote katika Al-Masihi Isa walio Filipi, pamoja na waangalizi na mashemasi. Neema na amani zinazotoka kwa Mungu, Baba yetu, na kwa Bwana wetu Isa Al-Masihi ziwe nanyi. Ninamshukuru Mungu wangu kila niwakumbukapo ninyi. Katika maombi yangu yote daima nimekuwa nikiwaombea ninyi nyote kwa furaha, kwa sababu ya kushiriki kwenu katika kueneza Injili, tangu siku ya kwanza hadi leo. Nina hakika kwamba yeye aliyeianza kazi njema mioyoni mwenu, ataiendeleza na kuikamilisha hata siku ya Al-Masihi Isa. Ni haki na ni wajibu wangu kufikiri hivi juu yenu nyote, kwa sababu ninyi mko moyoni mwangu. Ikiwa nimefungwa au nikiwa ninaitetea na kuithibitisha Injili, ninyi nyote mnashiriki neema ya Mungu pamoja nami. Mungu ni shahidi wangu jinsi ninavyowaonea shauku ninyi nyote kwa huruma ya Al-Masihi Isa.