Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mithali 29

29
1Anayekaza shingo baada ya maonyo mengi,
ataangamia ghafula, na kamwe hatapona.
2Wenye haki wanapostawi, watu hufurahi;
waovu watawalapo, watu hulia kwa huzuni.
3Mtu apendaye hekima huleta furaha kwa baba yake,
bali aambatanaye na makahaba hutapanya mali yake.
4Kwa haki mfalme huipa nchi uthabiti,
bali mfalme aliye na tamaa ya rushwa huiangamiza.
5Yeyote amsifuye jirani yake isivyostahili,
anautandaza wavu kuitega miguu yake.
6Mwovu hutegwa na dhambi yake mwenyewe,
bali mwenye haki hushangilia na kufurahi.
7Mwenye haki hujali haki kwa ajili ya maskini,
bali mwovu hajishughulishi na hilo.
8Wanaodhihaki huuchochea mji,
bali wenye hekima huzuia hasira.
9Mwenye hekima akienda mahakamani na mpumbavu,
mpumbavu hukasirika na kudhihaki, wala hakuna amani.
10Watu wanaomwaga damu humchukia mtu mwadilifu,
na hutafuta kumuua mtu mnyofu.
11Mpumbavu huonesha hasira yake yote,
bali mwenye hekima hujizuia.
12Mtawala akisikiliza uongo,
maafisa wake wote huwa waovu.
13Mtu maskini na mtu mdhalimu wanafanana kwa jambo hili:
Mwenyezi Mungu hutia nuru macho yao wote wawili.
14Kama mfalme akiwaamua maskini kwa haki,
kiti chake kitakuwa thabiti daima.
15Fimbo ya maonyo hutia hekima,
bali mtoto asiyeonywa humwaibisha mama yake.
16Waovu wanapostawi,
dhambi huongezeka pia;
lakini wenye haki wataliona anguko lao.
17Mkanye mwanao, naye atakupa amani;
atakuletea furaha unayotamani.
18Mahali pasipo na ufunuo, watu huacha kujizuia,
bali ana heri mtu yule anayeitii sheria.
19Mtumishi hawezi kuonywa kwa maneno matupu,
hata akielewa, hataitikia.
20Je, unamwona mtu azungumzaye kwa haraka?
Kuna matumaini zaidi kwa mpumbavu kuliko yeye.
21Kama mtu akimdekeza mtumishi wake tangu ujanani,
atamletea sikitiko mwishoni.
22Mtu mwenye hasira huchochea ugomvi,
naye mtu mwenye hasira ya haraka
hutenda dhambi nyingi.
23Kiburi cha mtu humshusha,
bali mtu mwenye roho ya unyenyekevu
hupata heshima.
24Anayekubaliana na mwizi ni adui wa nafsi yake mwenyewe;
huapishwa lakini hathubutu kushuhudia.
25Kuwaogopa watu huwa ni mtego,
bali yeyote amtumainiaye Mwenyezi Mungu atakuwa salama.
26Wengi hutafuta kusikilizwa na mtawala,
bali mtu hupata haki kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
27Mwenye haki huwachukia sana wasio waaminifu;
waovu huwachukia sana wenye haki.

Iliyochaguliwa sasa

Mithali 29: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia