Mithali 6:20-24
Mithali 6:20-24 NEN
Mwanangu, zishike amri za baba yako, wala usiyaache mafundisho ya mama yako. Yafunge katika moyo wako daima, yakaze kuizunguka shingo yako. Wakati utembeapo, yatakuongoza; wakati ulalapo, yatakulinda; wakati uamkapo, yatazungumza nawe. Kwa maana amri hizi ni taa, mafundisho haya ni mwanga na maonyo ya maadili ni njia ya uzima, yakikulinda na mwanamke aliyepotoka, kutokana na maneno laini ya mwanamke aliyepotoka.