Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 103

103
Zaburi 103
Upendo wa Mwenyezi Mungu
Zaburi ya Daudi.
1Ee nafsi yangu, umhimidi Mwenyezi Mungu.
Vyote vilivyo ndani yangu
vilihimidi jina lake takatifu.
2Ee nafsi yangu, umhimidi Mwenyezi Mungu,
wala usisahau wema wake wote:
3akusamehe dhambi zako zote,
akuponya magonjwa yako yote,
4aukomboa uhai wako na kaburi,
akuvika taji la upendo na huruma,
5atosheleza mahitaji yako kwa vitu vyema,
ili ujana wako uhuishwe kama wa tai.
6Mwenyezi Mungu hutenda haki,
naye huwapa hukumu ya haki
wote wanaodhulumiwa.
7Alimjulisha Musa njia zake,
na watu wa Israeli matendo yake.
8Mwenyezi Mungu ni mwingi wa huruma na mwenye neema;
si mwepesi wa hasira, bali amejaa upendo.
9Yeye hatalaumu siku zote,
wala haweki hasira yake milele,
10yeye hatutendei kulingana na dhambi zetu
wala hatupatilizi kwa kadiri ya maovu yetu.
11Kama vile mbingu zilivyo juu ya dunia,
ndivyo wema wake ulivyo mwingi kwa wanaomcha;
12kama mashariki ilivyo mbali na magharibi,
ndivyo Mungu alivyoziweka dhambi zetu mbali nasi.
13Kama baba alivyo na huruma kwa watoto wake,
ndivyo Mwenyezi Mungu anavyowahurumia wale wanaomcha;
14kwa kuwa anajua tulivyoumbwa,
anakumbuka kwamba sisi tu mavumbi.
15Kuhusu mwanadamu, siku zake ni kama majani,
anachanua kama ua la kondeni;
16upepo huvuma juu yake nalo hutoweka,
mahali pake hapalikumbuki tena.
17Lakini kutoka milele hata milele
upendo wa Mwenyezi Mungu uko kwa wale wamchao,
nayo haki yake kwa watoto wa watoto wao:
18kwa wale walishikao agano lake
na kukumbuka kuyatii mausia yake.
19Mwenyezi Mungu ameweka imara kiti chake cha enzi mbinguni,
na ufalme wake unatawala vitu vyote.
20Mhimidini Mwenyezi Mungu, enyi malaika wake,
ninyi mlio mashujaa, mnaozitii amri zake,
ninyi mnaotii neno lake.
21Mhimidini Mwenyezi Mungu, ninyi jeshi lake lote la mbinguni,
ninyi watumishi wake mnaofanya mapenzi yake.
22Mhimidini Mwenyezi Mungu, enyi kazi zake zote
kila mahali katika milki yake.
Ee nafsi yangu, umhimidi Mwenyezi Mungu.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 103: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia