Zaburi 139:1-12
Zaburi 139:1-12 NENO
Ee Mwenyezi Mungu, umenichunguza na kunijua. Unajua ninapoketi na ninapoinuka; unatambua mawazo yangu tokea mbali. Unafahamu kutoka kwangu na kulala kwangu; unaelewa njia zangu zote. Kabla neno halijafika katika ulimi wangu, wewe walijua kikamilifu, Ee Mwenyezi Mungu. Umenizingira nyuma na mbele; umeweka mkono wako juu yangu. Maarifa haya ni ya ajabu mno kwangu, ni ya juu sana kwangu kuyafikia. Niende wapi nijiepushe na Roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako? Nikienda juu mbinguni, wewe uko huko; nikifanya vilindi kuwa kitanda changu, wewe uko huko. Nikipanda juu kwa mabawa ya mapambazuko, nikikaa pande za mbali za bahari, hata huko mkono wako utaniongoza, mkono wako wa kuume utanishika kwa uthabiti. Nikisema, “Hakika giza litanificha na nuru inayonizunguka iwe usiku,” hata giza halitakuwa giza kwako, usiku utang’aa kama mchana, kwa kuwa giza ni kama nuru kwako.