Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 8:1-9

Zaburi 8:1-9 NENO

Ee Mwenyezi Mungu, Bwana wetu, tazama jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani kote! Umeuweka utukufu wako juu ya mbingu. Midomoni mwa watoto wachanga na wanaonyonya umeamuru sifa, kwa sababu ya watesi wako, kumnyamazisha adui na mlipiza kisasi. Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, mwezi na nyota, ulizoziratibisha, mwanadamu ni kitu gani hata unamfikiria, binadamu ni nani hata unamjali? Umemfanya chini kidogo kuliko viumbe wa mbinguni, ukamvika taji la utukufu na heshima. Umemfanya mtawala juu ya kazi za mikono yako; umeweka vitu vyote chini ya miguu yake. Mifugo na makundi yote pia, naam, na wanyama wa kondeni, ndege wa angani na samaki wa baharini, naam, kila kinachoogelea katika njia za bahari. Ee Mwenyezi Mungu, Bwana wetu, tazama jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani kote!