Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Warumi Utangulizi

Utangulizi
Paulo aliwaandikia watakatifu huko Rumi waraka huu. Wengi wa waumini wa kundi hili walikuwa ni watu wa Mataifa. Paulo anaanza kwa kueleza kwamba wanadamu wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo Wayahudi na watu wa Mataifa hawawezi kudai haki mbele za Mwenyezi Mungu, kwa sababu dhambi zao zinafuta haki hiyo. Lakini Mwenyezi Mungu, kwa neema yake, anatuhesabia haki tuliyoipoteza kwa dhambi, haki tunayoipata kupitia kwa kumwamini Mwanawe, Isa Al-Masihi. Kwa njia hii ya kuhesabiwa haki na Mwenyezi Mungu katika Mwanawe, tunaweza kuwa washindi katika maisha ya wafuasi wa Al-Masihi. Kisha Paulo anaeleza nafasi ya Wayahudi katika mpango wa Mwenyezi Mungu. Anamalizia waraka wake kwa kutoa maonyo kadha wa kadha kuhusu maadili.
Mwandishi
Mtume Paulo.
Kusudi
Paulo kujitambulisha kwa kundi la waumini la Rumi kwa ajili ya maandalizi ya safari yake, na pia ili kueleza kwa muhtasari msingi wa mafundisho yake.
Mahali
Korintho.
Tarehe
Mnamo 57 B.K.
Wahusika Wakuu
Mtume Paulo, na waumini wa Rumi.
Wazo Kuu
Mpango wa Mwenyezi Mungu wa wokovu na haki kwa wanadamu, kwa Wayahudi na pia watu wa Mataifa, kwa kuwa wote ni wenye dhambi (1:16-17).
Mambo Muhimu
Ufunuo kuhusu adhabu ya Mwenyezi Mungu dhidi ya dhambi, na haki ipatikanayo kupitia kwa imani kama msingi wa kuhesabiwa haki.
Yaliyomo
Utangulizi (1:1-17)
Watu wote hawana haki (1:18–3:20)
Haki ipatikanayo kwa kumwamini Al-Masihi (3:21–5:21)
Kushinda dhambi kwa uwezo wa Al-Masihi (6:1–8:39)
Mpango wa Mwenyezi Mungu kwa Israeli (9:1–11:36)
Misingi ya maisha ya wafuasi wa Al-Masihi (12:1–15:13)
Mipango ya Paulo na mawaidha ya mwisho (15:14–16:27).

Iliyochaguliwa sasa

Warumi Utangulizi: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia