Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zekaria 12:8-14

Zekaria 12:8-14 NEN

Katika siku hiyo, BWANA atawakinga wale waishio Yerusalemu, ili kwamba aliye dhaifu kupita wote miongoni mwao awe kama Daudi, nayo nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, kama Malaika wa BWANA akiwatangulia. Katika siku hiyo nitatoka kuangamiza mataifa yote yatakayoshambulia Yerusalemu. “Nami nitamiminia nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu roho ya neema na maombi. Watanitazama mimi, yule waliyemchoma. Nao watamwombolezea kama mtu anayemwombolezea mwanawe wa pekee na kusikitika kwa uchungu kama anayemsikitikia mzaliwa wake wa kwanza wa kiume. Katika siku hiyo kilio kitakuwa kikubwa Yerusalemu, kama kilio cha Hadad-Rimoni katika tambarare ya Megido. Nchi itaomboleza, kila ukoo peke yake, nao wake zao peke yao. Ukoo wa nyumba ya Daudi na wake zao, ukoo wa nyumba ya Nathani na wake zao, ukoo wa nyumba ya Lawi na wake zao, ukoo wa Shimei na wake zao, na koo zote zilizobaki na wake zao.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zekaria 12:8-14