Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Nya 23

23
Familia za Walawi na Wajibu wao
1 # 1 Fal 1:33; 1 Nya 28:5; 29:22-25 Basi Daudi alikuwa mzee, ameshiba siku; akamtawaza mwanawe Sulemani awe mfalme juu ya Israeli. 2Akawakusanya wakuu wote wa Israeli, pamoja na makuhani na Walawi. 3#Hes 4:3Nao wakahesabiwa Walawi wenye miaka thelathini na zaidi; na jumla yao kwa vichwa, mtu kwa mtu, ikapata thelathini na nane elfu. 4#Kum 16:18; 1 Nya 26:29; 2 Nya 19:8Katika hao ishirini na nne elfu walikuwa wa kusimamia kazi ya nyumba ya BWANA; na sita elfu walikuwa maakida na makadhi; 5#2 Nya 29:25,26; Amo 6:5na elfu nne walikuwa mabawabu; na elfu nne walimsifu BWANA kwa vinanda, nilivyovifanya, alisema Daudi, vya kumsifia. 6#Kut 6:16; Hes 26:57; 1 Nya 6:1; 2 Nya 8:14; 29:25; 31:2; 35:10; Ezr 6:18Basi Daudi akawagawanya kuwa zamu zao sawasawa na wana wa Lawi; Gershoni, Kohathi, na Merari. 7Wa Wagershoni; Ladani, na Shimei. 8Wana wa Ladani; Yehieli mkuu wao, na Zethamu, na Yoeli, watu watatu. 9Wana wa Shimei; Shelomothi, na Hazieli, na Harani, watatu. Hao walikuwa vichwa vya mbari za baba za Ladani. 10Na wana wa Shimei; Yahathi, na Zina, na Yeushi, na Beria. Hao wanne walikuwa wana wa Shimei. 11Naye Yahathi alikuwa mkubwa wao, na Zina alikuwa wa pili; lakini Yeushi na Beria hawakuwa na wana wengi; basi wakawa mbari ya baba kwa kuhesabiwa pamoja. 12#Kut 6:18; 1 Nya 6:2Wana wa Kohathi; Amramu, Ishari, Hebroni, na Uzieli, watu wanne. 13#Kut 28:1; Hes 18:1,7; Ebr 5:4; Kut 30:7; Law 10:1,2; Hes 16:40; 1 Sam 2:28; Kum 21:5; Hes 6:23Wana wa Amramu; Haruni na Musa; naye Haruni akatengwa, ili ayatakase yaliyo matakatifu sana, yeye na wanawe milele, ili kufukiza uvumba mbele za BWANA, kumtumikia, na kubariki kwa jina lake, milele. 14Lakini kwa habari za Musa, mtu wa Mungu, wanawe hutajwa miongoni mwa kabila ya Lawi. 15#Kut 2:22; 18:3,4Wana wa Musa; Gershomu na Eliezeri. 16Wana wa Gershomu; Shebueli mkuu wao. 17Na wana wa Eliezeri; Rehabia mkuu wao. Yeye Eliezeri hakuwa na wana wengine; lakini wana wa Rehabia walikuwa wengi sana. 18Wana wa Ishari; Shelomithi mkuu wao. 19Wana wa Hebroni; Yeria mkuu wao, Amaria wa pili, Yahazieli wa tatu, na Yekameamu wa nne. 20Wana wa Uzieli; Mika mkuu wao, na Ishia wa pili. 21Wana wa Merari; Mali na Mushi. Wana wa Mali; Eleazari, na Kishi. 22#Hes 36:6Akafa Eleazari, wala hakuwa na wana, ila binti tu; na ndugu zao, wana wa Kishi, wakawaoa. 23#1 Nya 24:30Wana wa Mushi; Mali, na Ederi, na Yeremothi, watu watatu. 24#Hes 10:17; 1:3; 4:3Hao walikuwa wana wa Lawi, kwa kufuata mbari za baba zao, yaani, vichwa vya mbari za baba zao waliohesabiwa, kwa hiyo hesabu ya majina yao kwa vichwa, hao walioifanya kazi ya utumishi wa nyumba ya BWANA, wenye miaka ishirini na zaidi. 25Kwa kuwa Daudi alisema, BWANA, Mungu wa Israeli, amewastarehesha watu wake; naye hukaa Yerusalemu milele; 26#Hes 4:5wala Walawi hawahitaji tena kuichukua maskani, na vyombo vyake vyote kwa utumishi wake. 27Maana kwa maneno ya mwisho ya Daudi, hao wana wa Lawi walihesabiwa, wenye miaka ishirini na zaidi. 28Kwani kazi yao ilikuwa kuwangojea wana wa Haruni katika utumishi wa nyumba ya BWANA, nyuani, na vyumbani, na kwa kuvisafisha vitakatifu vyote, ndiyo kazi ya utumishi wa nyumba ya Mungu; 29#Kut 25:30; Law 24:5-9; 1 Nya 9:29,32; Law 6:20; 2:4; 19:35tena kazi ya mikate ya wonyesho, na ya unga mwembamba wa sadaka ya unga; ikiwa ni wa maandazi yasiyochachwa, au wa yale yaliyotokoswa, au wa yale yaliyookwa; na kazi ya kila namna ya kipimo na cheo; 30#1 Nya 6:31-33; 9:33; 2 Nya 31:2; Zab 135:1,3,19,20; Ufu 5:8-14; 14:3nao wasimame kila asubuhi kumshukuru na kumsifu BWANA, na jioni vivyo hivyo; 31#Hes 10:10; Zab 81:3; Isa 1:13,14; Law 23:4na kumtolea BWANA sadaka zote za kuteketezwa, katika siku za sabato, za mwezi mpya, na za sikukuu zilizoagizwa, kwa hesabu kadiri ya agizo lake, daima mbele za BWANA; 32#Hes 1:53; 3:6tena walinde ulinzi wa hema ya kukutania, na ulinzi wa patakatifu, na ulinzi wa wana wa Haruni, ndugu zao, katika utumishi wa nyumba ya BWANA.

Iliyochaguliwa sasa

1 Nya 23: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia