Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Fal 19:11-14

1 Fal 19:11-14 SUV

Akasema, Toka, usimame mlimani mbele za BWANA. Na tazama, BWANA akapita; upepo mwingi wa nguvu ukaipasua milima, ukaivunja-vunja miamba mbele za BWANA; lakini BWANA hakuwamo katika upepo ule; na baada ya upepo, tetemeko la nchi; lakini BWANA hakuwamo katika lile tetemeko la nchi; na baada ya tetemeko la nchi kukawa na moto; lakini BWANA hakuwamo katika moto ule; na baada ya moto sauti ndogo, ya utulivu. Ikawa, Eliya alipoisikia, alijifunika uso wake katika mavazi yake, akatoka, akasimama mlangoni mwa pango. Na tazama, sauti ikamjia, kusema, Unafanya nini hapa, Eliya? Akasema, Nimeona wivu mwingi kwa ajili ya BWANA, Mungu wa majeshi; kwa kuwa wana wa Israeli wameyaacha maagano yako, na kuzivunja madhabahu zako, na kuwaua manabii wako kwa upanga; nami nimesalia, mimi peke yangu; nao wanitafuta roho yangu waiondoe.