1
Salamu
1 #
Yak 1:1
Petro, mtume wa Yesu Kristo, kwa wateule wa Utawanyiko, wakaao hali ya ugeni katika Ponto, na Galatia, na Kapadokia, na Asia, na Bithinia; 2#Rum 8:29; Ebr 12:24kama vile Mungu Baba alivyotangulia kuwajua katika kutakaswa na Roho, hata mkapata kutii na kununyiziwa damu ya Yesu Kristo. Neema na amani na ziongezwe kwenu.
Tumaini Hai
3 #
Yak 1:18
Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu; 4#Kol 1:12tupate na urithi usioharibika, usio na uchafu, usionyauka, uliotunzwa mbinguni kwa ajili yenu. 5#Yn 10:28; 17:11; Rum 5:3,4; Gal 3:23; 1 Kor 2:5Nanyi mnalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani hata mpate wokovu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho. 6#1 Pet 5:10; Ebr 12:11; Yak 1:2; 2 Kor 4:17Mnafurahi sana wakati huo, ijapokuwa sasa kwa kitambo kidogo, ikiwa ni lazima, mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali; 7#Mit 17:3; Mal 3:3; Rum 2:7,10; Yak 1:3ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo. 8#Yn 17:20; 20:29; 2 Kor 5:7; 2 Tim 4:8Naye mwampenda, ijapokuwa hamkumwona; ambaye ijapokuwa hamwoni sasa, mnamwamini; na kufurahi sana, kwa furaha isiyoneneka, yenye utukufu, 9#Rum 6:22katika kuupokea mwisho wa imani yenu, yaani, wokovu wa roho zenu. 10#Mt 13:17; Lk 10:24Katika habari ya wokovu huo manabii walitafuta-tafuta na kuchunguza-chunguza, ambao walitabiri habari za neema itakayowafikia ninyi. 11#Zab 22:1; Isa 52:13—53:12; Lk 24:26Wakatafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao, ambaye alitangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwako baada ya hayo. 12#Efe 3:10; Lk 2:13Wakafunuliwa ya kuwa si kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yenu walihudumu katika mambo hayo, ambayo sasa yamehubiriwa kwenu na wale waliowahubiri ninyi Injili kwa Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni. Mambo hayo malaika wanatamani kuyachungulia.
Wito wa Kuishi Maisha ya Utakatifu
13 #
Lk 12:35; Efe 6:14 Kwa hiyo vifungeni viuno vya nia zenu, na kuwa na kiasi; mkiitumainia kwa utimilifu ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wake Yesu Kristo. 14#Rum 12:2; Efe 2:3; 4:17Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu; 15bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; 16#Law 11:44-45; 19:2; 20:7kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu. 17#Zab 89:26; Yer 3:19; Mal 1:6; Mt 6:9; Rum 2:11Na ikiwa mnamwita Baba, yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, enendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni. 18#Isa 52:3; 1 Kor 6:20; 7:23Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu; 19#Isa 53:7; Ebr 9:14bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo. 20#Rum 16:25; Efe 1:4Naye amejulikana kweli tangu zamani, kabla haijawekwa misingi ya dunia; lakini alifunuliwa mwisho wa zamani kwa ajili yenu; 21#Yn 14:6; Rum 4:24; Kol 1:27ambao kwa yeye mmekuwa wenye kumwamini Mungu, aliyemfufua katika wafu akampa utukufu; hata imani yenu na tumaini lenu liwe kwa Mungu. 22#1 Yoh 5:1Mkiisha kujitakasa roho zenu kwa kuitii kweli, hata kuufikilia upendano wa ndugu usio na unafiki, basi jitahidini kupendana kwa moyo. 23#Dan 6:26; Yn 1:13; Yak 1:18Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele. 24#Isa 40:6-8; Yak 1:10,11Maana,
Mwili wote ni kama majani,
Na fahari yake yote ni kama ua la majani.
Majani hukauka na ua lake huanguka;
25 #
Isa 40:8
Bali Neno la Bwana hudumu hata milele.
Na neno hilo ni neno lile jema lililohubiriwa kwenu.