Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Nya 21

21
Yehoramu Atawala
1Yehoshafati akalala na babaze, akazikwa pamoja na babaze katika mji wa Daudi; akatawala Yehoramu mwanawe mahali pake. 2Naye alikuwa na ndugu, wana wa Yehoshafati, Azaria, na Yehieli, na Zekaria, na Azaria, na Mikaeli, na Shefatia; hao wote walikuwa wana wa Yehoshafati mfalme wa Israeli. 3Baba yao akawapa zawadi kubwa, za fedha, na za dhahabu, na za tunu, pamoja na miji yenye maboma katika Yuda; lakini ufalme akampa Yehoramu, kwa sababu alikuwa mzaliwa wa kwanza. 4#Mwa 4:8; Amu 9:5; 1 Yoh 3:12Basi Yehoramu alipoinuliwa juu ya ufalme wa babaye, na kujitia nguvu, akawaua nduguze wote kwa upanga, na baadhi ya wakuu wa Israeli pia. 5Yehoramu alikuwa na umri wa miaka thelathini na miwili alipoanza kutawala, akatawala miaka minane huko Yerusalemu. 6#2 Fal 8:18; 2 Nya 18:1; 22:2; Neh 13:26Akaiendea njia ya wafalme wa Israeli, kama walivyofanya nyumba ya Ahabu; kwa kuwa alikuwa amemwoa binti Ahabu; akafanya maovu machoni pa BWANA. 7#2 Sam 7:12,13; 1 Fal 11:36; 2 Fal 8:19; Zab 132:11Walakini BWANA hakupenda kuiharibu nyumba ya Daudi, kwa sababu ya agano alilolifanya na Daudi, na kama alivyomwahidi kuwa atampa taa, yeye na wazao wake siku zote.
Uasi wa Edomu
8 # Mwa 27:40; 2 Fal 8:20; 9:22; Zab 106:39; Ufu 17:1-5 Zamani zake Edomu wakaasi chini ya mkono wa Yuda, wakajifanyia mfalme. 9Ndipo akavuka Yehoramu na maakida wake, na magari yake yote pamoja naye; akaondoka usiku, akawapiga Waedomi waliomzunguka yeye na hao maakida wa magari. 10#Mwa 27:40Hivyo Edomu wakaasi chini ya mkono wa Yuda, hata leo; wakaasi na Libna zamani zizo hizo chini ya mkono wake: kwa sababu alikuwa amemwacha BWANA, Mungu wa baba zake.
Barua ya Eliya
11 # Law 17:7; 20:5 Tena ndiye aliyefanya mahali pa juu milimani pa Yuda, na kuwaendesha katika uasherati wenyeji wa Yerusalemu, na kuwakosesha Yuda. 12Likamjia andiko kutoka kwa Eliya nabii, kusema, BWANA, Mungu wa Daudi baba yako, asema hivi, Kwa sababu hukuziendea njia za Yehoshafati baba yako, wala njia za Asa mfalme wa Yuda; 13#Kut 34:15; 2 Fal 9:22lakini umeiendea njia ya wafalme wa Israeli, ukawaendesha katika uasherati Yuda na wenyeji wa Yerusalemu, kama walivyofanya nyumba ya Ahabu; tena umewaua ndugu zako wa nyumba ya baba yako, waliokuwa wema kuliko wewe; 14tazama, BWANA atawapiga pigo kubwa watu wako, na watoto wako, na wake zako, na mali yako yote; 15nawe utakuwa na ugonjwa mkuu kwa maradhi ya matumbo, yatakapotokea matumbo yako kwa sababu ya ugonjwa huo siku kwa siku. 16#2 Sam 24:1; 1 Fal 11:14,23; 2 Nya 22:1BWANA akawaamsha roho Wafilisti, na Waarabu waliowaelekea Wakushi juu ya Yehoramu, 17#2 Nya 24:7nao wakakwea juu ya nchi ya Yuda, wakaipenya, wakaichukua mali yote iliyoonekama nyumbani mwa mfalme, na wanawe pia, na wakeze; asisaziwe mwana hata mmoja, ila Ahazia,#21:17 Au, Yehoahazi. aliyekuwa mdogo miongoni mwa wanawe.
Ugonjwa na Kifo cha Yehoramu
18Na baada ya hayo yote BWANA akampiga matumbo kwa ugonjwa usioponyeka. 19Ikawa baada ya siku, ikiisha miaka miwili, matumbo yake yakatokea kwa sababu ya ugonjwa wake, akafa akiugua vibaya. Wala watu wake hawakumfukizia mafukizo kama ya baba zake. 20Alikuwa na umri wa miaka thelathini na miwili alipoanza kutawala, akatawala huko Yerusalemu miaka minane; akafariki bila kutamaniwa; wakamzika mjini mwa Daudi, ila si katika makaburi ya wafalme.

Iliyochaguliwa sasa

2 Nya 21: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia