8
Sauli Atesa Kanisa
1 #
Mdo 7:58; 11:19; 22:20 Siku ile kukatukia adha kuu ya kanisa lililokuwa katika Yerusalemu; wote wakatawanyika katika nchi ya Uyahudi na Samaria, isipokuwa hao mitume. 2#Mt 14:12Watu watauwa wakamzika Stefano, wakamfanyia maombolezo makuu. 3#Mdo 22:4-5; 9:1; 26:9-11Sauli akaliharibu kanisa, akiingia kila nyumba, na kuwaburuta wanaume na wanawake na kuwatupa gerezani.
Filipo Ahubiri katika Samaria
4Lakini wale waliotawanyika wakaenda huko na huko wakilihubiri neno. 5#Mdo 6:5Filipo akatelemka akaingia mji wa Samaria, akawahubiri Kristo. 6Na makutano kwa nia moja wakasikiliza maneno yale yaliyosemwa na Filipo walipoyasikia na kuziona ishara alizokuwa akizifanya. 7#Mk 16:17Kwa maana pepo wachafu wakawatoka wengi waliopagawa nao, wakilia kwa sauti kuu; na watu wengi waliopooza, na viwete, wakaponywa. 8#Yn 4:40-42Ikawa furaha kubwa katika mji ule.
9Na mtu mmoja, jina lake Simoni, hapo kwanza alikuwa akifanya uchawi katika mji ule, akiwashangaza watu wa taifa la Wasamaria, akisema ya kuwa yeye ni mtu mkubwa. 10Wote wakamsikiliza tangu mdogo hata mkubwa, wakisema, Mtu huyu ni uweza wa Mungu, ule Mkuu. 11Wakamsikiliza, kwa maana amewashangaza muda mwingi kwa uchawi wake. 12#Mt 28:19Lakini walipomwamini Filipo, akizihubiri habari njema za ufalme wa Mungu, na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake. 13Na yeye Simoni mwenyewe aliamini akabatizwa, akashikamana na Filipo; akashangaa alipoziona ishara na miujiza mikubwa inayotendeka.
14 #
Mdo 3:1
Na mitume waliokuwako Yerusalemu, waliposikia ya kwamba Samaria imelikubali neno la Mungu, wakawapelekea Petro na Yohana; 15ambao waliposhuka, wakawaombea wampokee Roho Mtakatifu; 16kwa maana bado hajawashukia hata mmoja wao, ila wamebatizwa tu kwa jina lake Bwana Yesu. 17#1 Tim 4:14Ndipo wakaweka mikono yao juu yao, nao wakampokea Roho Mtakatifu.
18Hata Simoni alipoona ya kuwa watu wanapewa Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono ya mitume, akataka kuwapa fedha akisema, 19Nipeni na mimi uwezo huu, ili kila mtu nitakayemweka mikono yangu, apokee Roho Mtakatifu. 20Lakini Petro akamwambia, Fedha yako na ipotelee mbali pamoja nawe, kwa kuwa umedhania ya kuwa karama ya Mungu yapatikana kwa mali. 21#Zab 78:37; Efe 5:5Huna fungu wala huna sehemu katika jambo hili, kwa kuwa moyo wako si mnyofu mbele za Mungu. 22Basi, tubia uovu wako huu, ukamwombe Bwana, ili kama yamkini, usamehewe fikira hii ya moyo wako. 23#Kum 29:18; Isa 58:6; Ebr 12:15Kwa maana nakuona u katika uchungu kama nyongo, na tena u katika kifungo cha uovu. 24Simoni akajibu, akasema, Niombeeni ninyi kwa Bwana, yasinifikilie mambo haya mliyosema hata moja.
25Nao walipokwisha kushuhudia na kulihubiri neno la Bwana wakarudi Yerusalemu, wakaihubiri Injili katika vijiji vingi vya Wasamaria.
Filipo na Towashi wa Ethiopia
26Malaika wa Bwana akasema na Filipo, akamwambia, Ondoka ukaende upande wa kusini hata njia ile itelemkayo kutoka Yerusalemu kwenda Gaza; nayo ni jangwa.
27 #
Isa 56:3-7
Naye akaondoka, akaenda; mara akamwona mtu wa Kushi, towashi, mwenye mamlaka chini ya Kandake malkia wa Kushi, aliyewekwa juu ya hazina yake yote; naye alikuwa amekwenda Yerusalemu kuabudu, 28akawa akirejea, ameketi garini mwake akisoma chuo cha nabii Isaya. 29Roho akamwambia Filipo, Sogea karibu na gari hili, ukashikamane nalo. 30Basi Filipo akaenda mbio, akamsikia anasoma chuo cha nabii Isaya; akanena, Je! Yamekuelea haya unayosoma? 31#Yn 16:13Akasema, Nitawezaje kuelewa, mtu asiponiongoza? Akamsihi Filipo apande na kuketi pamoja naye. 32#Isa 53:7-8Na fungu la Maandiko alilokuwa akilisoma ni hili,
Aliongozwa kwenda machinjoni kama kondoo,
Na kama vile mwana-kondoo alivyo kimya mbele yake amkataye manyoya,
Vivyo hivyo yeye naye hafunui kinywa chake.
33Katika kujidhili kwake hukumu yake iliondolewa.
Ni nani atakayeeleza kizazi chake?
Kwa maana uzima wake umeondolewa katika nchi.
34Yule towashi akamjibu Filipo, akasema, Nakuomba, nabii huyu; asema maneno haya kwa habari ya nani; ni habari zake mwenyewe au za mtu mwingine? 35Filipo akafunua kinywa chake, naye, akianza kwa andiko lilo hilo, akamhubiri habari njema za Yesu. 36#Mdo 10:47Wakawa wakiendelea njiani, wakafika mahali penye maji; yule towashi akasema, Tazama, maji haya; ni nini kinachonizuia nisibatizwe? [ 37Filipo akasema, Ukiamini kwa moyo wako wote, inawezekana. Akajibu, akanena, Naamini ya kwamba Yesu Kristo ndiye Mwana wa Mungu.] 38Akaamuru lile gari lisimame; wakatelemka wote wawili majini, Filipo na yule towashi; naye akambatiza. 39#1 Fal 18:12Kisha, walipopanda kutoka majini, Roho wa Bwana akamnyakua Filipo, yule towashi asimwone tena; basi alikwenda zake akifurahi. 40#Mdo 21:8,9Lakini Filipo akaonekana katika Azoto, na alipokuwa akipita akahubiri Injili katika miji yote, hata akafika Kaisaria.