Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kum 2

2
1 # Hes 21:4 Ndipo tukageuka, tukashika safari yetu kwenda jangwani kwa njia ya Bahari ya Shamu, kama alivyoniambia BWANA; tukawa kuizunguka milima ya Seiri siku nyingi. 2BWANA akanena, akaniambia, 3Mlivyouzunguka mlima huu vyatosha; geukeni upande wa kaskazini. 4#Mwa 36:8Nawe waagize watu, uwaambie, Mtapita kati ya mpaka wa ndugu zenu wana wa watu, uwaambie, Mtapita kati ya mpaka wa ndugu zenu wana wa Esau waketio Seiri; nao watawaogopa; basi jiangalieni nafsi zenu sana; 5#Mwa 36:8; Kum 32:8; Yos 24:4; 2 Nya 20:10-12; Zab 115:3; 135:5,6; Dan 4:32,35; Mdo 17:26msitete nao; kwa maana sitawapa katika nchi yao kamwe, hata kiasi cha kukanyaga wayo wa mguu; kwa kuwa nimempa Esau milima ya Seiri kuwa milki yake. 6Nunueni vyakula kwao kwa fedha, mpate kula; na maji nayo nunueni kwao kwa fedha, mpate kunywa. 7Kwa kuwa BWANA, Mungu wako, amekubarikia katika kazi yote ya mkono wako; amejua ulivyotembea katika jangwa kubwa hili; miaka arobaini hii alikuwa nawe BWANA, Mungu wako; hukukosa kitu. 8#1 Fal 9:26; 2 Fal 14:22; 16:6Basi tukapita kando yao ndugu zetu wana wa Esau, waketio Seiri kutoka njia ya Araba, kutoka Elathi na kutoka Esion-geberi.
Tukageuka tukapita njia ya bara ya Moabu. 9#Mwa 19:37; Hes 21:28; Zab 83:8BWANA akaniambia, usiwasumbue Wamoabi, wala usishindane nao katika mapigano; kwa kuwa sitakupa katika nchi yake kuimiliki; kwa sababu Ari nimewapa wana wa Lutu kuimiliki. 10#Mwa 14:5; Hes 13:22; Kum 9:2(Walioketi humo hapo kale ni Waemi, nao ni watu wakubwa, wengi, warefu, mfano wa Waanaki; 11na hawa nao wadhaniwa kuwa majitu#2:11 Au, Warefai. kama Waanaki; lakini Wamoabi huwaita Waemi. 12#Mwa 14:6; 36:20; 1 Nya 1:38-42Na Wahori nao walikuwa wakikaa Seiri hapo kale, lakini wana wa Esau waliwafuata; wakawaangamiza mbele yao, wakakaa badala yao; kama alivyofanya Israeli nchi ya milki yake aliyopewa na BWANA.) 13Sasa basi ondokeni, mkakivuke kijito cha Zeredi. Nasi tukakivuka kile kijito cha Zeredi. 14#Hes 14:28-35; 26:64; 32:11; Zab 78:33; 90:3-9; Kum 1:34,35; Eze 20:15Na siku tulizokuwa tukienda kutoka Kadesh-barnea hata tulipovuka kijito cha Zeredi, zilikuwa ni miaka thelathini na minane; maana, hata walipokwisha kuangamizwa watu wa vita kutoka kati ya marago, kizazi chao chote, kama walivyoapiwa na BWANA. 15#1 Sam 5:6-11; 7:13; Zab 95:10,11; 106:26; Ebr 3:11-19; 4:1-5Tena mkono wa BWANA ulikuwa juu yao ili kuwaangamiza, kuwatoa kati ya marago, hata walipokoma.
16Basi ikawa, walipokwisha angamizwa kwa kufa watu wote wa vita kati ya watu, 17BWANA aliniambia, akasema, 18Hivi leo ivuke Ari, mpaka wa Moabu; 19#Mwa 19:38; 14:5na utakaposongea kuwaelekea wana wa Amoni, usiwasumbue wana wa Amoni, wala usishindane nao; kwa kuwa sitakupa katika nchi ya hao wana wa Amoni kuwa milki yako; kwa sababu nimewapa wana wa Lutu iwe milki yao. 20(Nchi hiyo nayo yadhaniwa kuwa ni nchi ya Warefai, hapo kale Warefai walikaa humo; lakini Waamoni huwaita Wazamzumi; 21nao ni watu wengi, wakubwa, warefu, kama Waanaki; lakini BWANA aliwaangamiza mbele yao; wakawafuata wakakaa badala yao; 22#Mwa 36:8; Ayu 12:23kama vile alivyowafanyia wana wa Esau, waliokaa Seiri, alipowaangamiza Wahori mbele yao; wakawafuata, wakakaa badala yao hata hivi leo; 23#Yos 13:3; Yer 25:20; Sef 2:4; Mwa 10:14; Amo 9:7na Waavi waliokuwa wakikaa katika vijiji mpaka Gaza waliangamizwa na Wakaftori waliotoka Kaftori, na hawa wakakaa badala yao.) 24#Hes 21:13,14; Amu 11:18Ondokeni, mshike safari yenu, mvuke bonde la Arnoni; tazama, nimemtia Sihoni Mwamori mfalme wa Heshboni mkononi mwako, na nchi yake; anzeni kuimiliki, mshindane naye katika mapigano. 25#Kut 15:14; Kum 11:25; Yos 2:9Hivi leo nitaanza mimi kutia utisho wako na kuhofiwa kwako juu ya watu walio chini ya mbingu kila mahali, watakaosikia uvumi wako, na kutetemeka, na kuingiwa na uchungu kwa sababu yako.
Kushindwa kwa Mfalme Sihoni
26 # Kum 20:10; Est 9:30 Nikatuma wajumbe kutoka bara ya Kedemothi kwenda kwa Sihoni mfalme wa Heshboni na maneno ya amani, kusema. 27#Hes 21:21; Amu 11:19Nipishe katikati ya nchi yako; nitakwenda kwa njia ya barabara, sitageuka kwenda mkono wa kuume wala wa kushoto. 28#Hes 20:19Nawe uniuzie chakula kwa fedha nile; unipe na maji kwa fedha, ninywe; ila unipishe katikati kwa miguu yangu, hayo tu; 29#Kum 23:3; Amu 11:17kama walivyonifanyia hao wana wa Esau waketio Seiri, na hao Wamoabi waketio Ari; hata nivuke Yordani niingie nchi tupewayo na BWANA, Mungu wetu. 30#Hes 21:23; Yos 11:19,20; Kut 4:21; Hos 4:17; Yak 1:13-15Lakini Sihoni mfalme wa Heshboni hakutuacha kupitia kwake; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, alimfanya mgumu roho yake, akamtia ukaidi moyoni mwake, apate mtia mkononi mwako kama alivyo hivi leo. 31Kisha BWANA akaniambia, Tazama, nimeanza kumtoa Sihoni na nchi yake mbele yako; anza kuimiliki, upate kuirithi nchi yake. 32Ndipo Sihoni alipotutokea juu yetu yeye na watu wake wote, kupigana huko Yahasa. 33#Kut 23:31; Kum 7:2; 20:16; Zab 135:10-12; 136:18-20; Kum 29:7BWANA, Mungu wetu, akamtoa mbele yetu, tukampiga yeye na wanawe, na watu wake wote. 34#Law 27:28; Hes 21:2,3; Kum 7:2,26; Yos 7:11; 8:25,26; 9:24; 11:14; 1 Sam 15:3-9Tukatwaa miji yake yote wakati huo, tukaharibu kabisa kila mji uliokuwa na watu, pamoja na wanawake na wadogo; tusimsaze hata mmoja; 35ila ng’ombe zao tuliwatwaa kuwa mawindo yetu, pamoja na nyara za miji tuliyoitwaa. 36#Kum 3:12; 4:48; Yos 13:9; Zab 44:3Kutoka Aroeri iliyo katika ukingo wa bonde la Arnoni, na huo mji ulio ndani ya bonde, mpaka kufika Gileadi, hapakuwa na mji uliokuwa mrefu kutushinda; BWANA, Mungu wetu, aliiweka wazi yote mbele yetu; ila nchi ya wana wa Amoni hukuisongelea; 37#Mwa 32:22; Hes 21:24; Kum 3:16upande wote wa mto wa Yaboki, na miji ya nchi ile ya milimani, na kila mahali alipotukataza BWANA, Mungu wetu.

Iliyochaguliwa sasa

Kum 2: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia