Mhu 3
3
Kila jambo na Wakati wake
1 #
Mhu 8:6
Kwa kila jambo kuna majira yake,
Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.
2 #
Mwa 47:29; Ayu 7:1; Isa 38:1; Yn 11:14; Ebr 9:27 Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa;
Wakati wa kupanda, na wakati wa kung’oa yaliyopandwa;
3 #
Mwa 9:6; 1 Sam 2:6; Hos 6:1,2 Wakati wa kuua, na wakati wa kupoza;
Wakati wa kubomoa, na wakati wa kujenga;
4 #
Kut 15:20; 2 Sam 6:16; Zab 149:3 Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka;
Wakati wa kuomboleza, na wakati wa kucheza;
5Wakati wa kutupa mawe, na wakati wa kukusanya mawe;
Wakati wa kukumbatia, na wakati wa kutokumbatia;
6Wakati wa kutafuta, na wakati wa kupoteza;
Wakati wa kuweka, na wakati wa kutupa;
7 #
Amo 5:13
Wakati wa kurarua, na wakati wa kushona;
Wakati wa kunyamaza, na wakati wa kunena;
8 #
Lk 14:26
Wakati wa kupenda, na wakati wa kuchukia;
Wakati wa vita, na wakati wa amani.
Kazi Tupewayo na Mungu
9 #
Mhu 1:3
Je! Mtendaji anayo faida gani katika yale anayojishughulisha nayo? 10#Mhu 1:13Nimeiona taabu ambayo Mungu amewapa wanadamu, ili kutaabika ndani yake. 11#Kum 32:4; Mhu 8:17; Rum 11:33Kila kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake; tena ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao; ila kwa jinsi mwanadamu asivyoweza kuivumbua kazi ya Mungu anayoifanya, tangu mwanzo hata mwisho.
12Mimi najua ya kwamba hakuna jema kwao kupita kufurahi, na kufanya mema maadamu wanaishi. 13#Mhu 2:24Tena ni karama ya Mungu kila mtu apate kula na kunywa, na kujiburudisha kwa mema katika kazi yake yote. 14#Yak 1:17Najua ya kwamba kila kazi aifanyayo Mungu itadumu milele; haiwezekani kuizidisha kitu, wala kuipunguza kitu; nayo Mungu ameifanya ili watu wamche Yeye. 15#Mhu 1:9Yale yaliyoko yamekuwako; na hayo yatakayokuwako yamekwisha kuwako; naye Mungu huyatafuta tena mambo yale yaliyopita.
Hukumu na Maisha ya baadaye ni ya Mungu
16 #
Mhu 5:8
Zaidi ya hayo, nikaona tena chini ya jua ya kwamba,
Mahali pa hukumu upo uovu,
Na mahali pa haki upo udhalimu.
17 #
Ayu 34:11; Mt 16:27; Rum 2:6; 2 Kor 5:10; 2 The 1:6 Nikasema moyoni mwangu, Mungu atawahukumu wenye haki na wasio haki; kwa kuwa kuna wakati huko kwa kila kusudi na kwa kila kazi. 18Nikasema moyoni mwangu, Ni kwa sababu ya wanadamu, ili Mungu awajaribu, nao waone ya kuwa wao wenyewe wafanana na wanyama. 19#Zab 49:12Kwa maana linalowatukia wanadamu linawatukia wanyama; jambo moja lawatukia; anavyokufa huyu ndivyo anavyokufa huyu; naam, wote wanayo pumzi moja; wala mwanadamu hana kitu cha kumpita mnyama; kwa maana yote ni ubatili. 20#Mwa 3:19Wote huendea mahali pamoja; wote hutoka katika mavumbi; na hata mavumbini hurudi tena. 21Ni nani ajuaye kama roho ya binadamu huenda juu, na kama roho ya mnyama huenda chini? 22#Mhu 2:10Hivyo nikaona ya kwamba hakuna jema kupita mwanadamu kuzifurahia kazi zake; kwa sababu hili ni fungu lake; kwa maana ni nani atakayemrudisha tena ili ayaone yatakayomfuata baadaye.
Iliyochaguliwa sasa
Mhu 3: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.