Est UTANGULIZI
UTANGULIZI
Esta ni mwanamke Myahudi ambaye alikuwa Malkia wa Uajemi na alihusika katika mpango mahsusi wa kuwaokoa Wayahudi wasiangamizwe (2:5-18). Esta ambaye alikuwa yatima alilelewa na ami wake Mordekai wa kabila la Benyamini. Mordekai alichukuliwa uhamishoni Babeli, baadaye aliishi Susa mji mkuu wa dola ya Uajemi.
Mwandishi wa Kitabu hiki anasimulia habari zilizomo kitabuni kwa uangalifu mwingi. Anaeleza hali na tabia ya mfalme Ahasuero, mke wake mfalme na jinsi Esta alivyopata kuwa malkia wa Uajemi.
Shabaha ya masimulizi haya ni kueleza jinsi watu wa Mungu walivyoshika imani yao wakiwa katika nchi ya kigeni. Vile vile simulizi la kitabu hicho, kwa namna moja au nyingine, kilikuwa na shabaha ya kuonyesha asili na chanzo cha sikukuu ya Purimu ambayo iliadhimishwa kabla ya Pasaka.
Yaliyomo:
1. Esta kuwa Malkia, Sura 1–2
2. Njama za Hamani, Sura 3–5
3. Hamani auawa, Sura 6–7
4. Wayahudi wawashinda maadui wao, Sura 8–10
Iliyochaguliwa sasa
Est UTANGULIZI: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.