Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kut 33

33
Agizo la Kuondoka Sinai
1 # Mwa 12:7; 26:3; 28:13 BWANA akanena na Musa, Haya, ondokeni, katokeni hapo, wewe na hao watu uliowaleta wakwee kutoka nchi ya Misri, waende nchi hiyo niliyomwapia Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, niliposema, Nitakipa kizazi chako nchi hii; 2#Kum 7:22; Yos 24:11nami nitamtuma malaika aende mbele yako; nami nitawafukuza Mkanaani, na Mwamori, na Mhiti, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi; 3#Kut 32:9; Kum 9:6waifikilie nchi imiminikayo maziwa na asali; kwa maana mimi sitakwenda kati yenu; kwa sababu ninyi ni watu wenye shingo ngumu; nisiwaangamize ninyi katika njia. 4#2 Sam 19:24Watu waliposikia habari hizo mbaya wakaomboleza wala hapana mtu aliyevaa vyombo vyake vya uzuri. 5#Zab 139:23BWANA akamwambia Musa, Waambie wana wa Israeli, Ninyi ni watu wenye shingo ngumu; kama mimi nikiingia kati yenu dakika moja, nitawaangamiza; basi sasa vueni vyombo vyenu vya uzuri ili nipate kujua nitakalowatenda. 6Basi wana wa Israeli wakavua vyombo vyao vyote vya uzuri, tangu mlima wa Horebu na mbele.
Hema nje ya Kambi
7 # 2 Sam 21:1 Basi desturi ya Musa, ilikuwa kuitwaa ile hema, na kuikita nje ya marago mbali na hayo marago; akaiita, hema ya kukutania. Hata kila mtu aliyekuwa akitaka neno kwa BWANA, akatoka, akaenda hata hema ya kukutania, iliyokuwa nje ya marago. 8#Hes 16:27Hata Musa alipotoka kuiendea ile hema, watu wote waliondoka wakasimama, kila mtu mlangoni pa hema yake, akamtazama Musa, hata alipokwisha kuingia hemani. 9#Zab 99:7Ikawa Musa alipoingia humo hemani, ile nguzo ya wingu ikashuka, ikasimama mlangoni pa ile hema; naye BWANA akasema na Musa. 10Watu wote wakaiona nguzo ya wingu ikisimama penye mlango wa hema; watu wote wakaondoka wakasujudu, kila mtu mlangoni pa hema yake. 11#Mwa 32:30; Kum 5:24; 34:10; Kut 24:13Naye BWANA akasema na Musa uso kwa uso, kama vile mtu asemavyo na rafiki yake. Kisha akageuka akarejea hata maragoni; bali mtumishi wake Yoshua, mwana wa Nuni, naye ni kijana, hakutoka mle hemani.
Maombezi ya Musa kwa Mungu
12 # Zab 1:6; Yer 1:5; Yn 10:14; 2 Tim 2:19 Musa akamwambia BWANA, Angalia, wewe waniambia, Wachukue watu hawa; nawe hukunijulisha ni nani utakayemtuma pamoja nami. Walakini umesema, Nakujua jina lako, nawe umepata neema mbele zangu. 13#Kut 34:9; Zab 25:4; 27:11; Kum 9:26; Yoe 2:17Basi, sasa nakuomba, ikiwa nimepata neema mbele zako, unionyeshe njia zako, nipate kukujua, ili nipate neema mbele zako; ukakumbuke ya kuwa taifa hilo ndilo watu wako. 14#Kut 40:34-38; Isa 63:9; Kum 3:20; Yos 21:44; 22:4; 23:1; Zab 95:11Akasema, Uso wangu utakwenda pamoja nawe, nami nitakupa raha. 15#Kut 34:9Naye akamwambia, Uso wako usipokwenda pamoja nami, usituchukue kutoka hapa. 16#Hes 14:14; Kum 4:34; 2 Sam 7:23; Zab 147:20; Tit 2:14Kwa maana itajulikanaje kuwa nimepata neema mbele zako, mimi na watu wako? Siyo kwa sababu unakwenda pamoja nasi, hata mimi na watu wako tutengwe na watu wote walio juu ya uso wa nchi? 17#Mwa 19:21; Yak 5:16BWANA akamwambia Musa, Nitafanya na neno hili ulilolinena, kwa maana umepata neema mbele zangu, nami nakujua jina lako. 18#1 Tim 6:16Akasema, Nakusihi unionyeshe utukufu wako. 19#Rum 9:1,15; 4:4; Yer 31:14Akasema, Nitapitisha wema wangu wote mbele yako, nami nitalitangaza jina la BWANA mbele yako; nami nitamfadhili yeye nitakayemfadhili; nitamrehemu yeye nitakayemrehemu. 20#Mwa 32:30; Kum 5:24; Amu 13:22; Isa 6:5; Ufu 1:16Kisha akasema, Huwezi kuniona uso wangu, maana mwanadamu hataniona akaishi. 21BWANA akasema, Tazama, hapa pana mahali karibu nami, nawe utasimama juu ya mwamba; 22#Isa 2:21; Zab 91:1,4kisha itakuwa wakati unapopita utukufu wangu, nitakutia katika ufa wa ule mwamba, na kukufunika kwa mkono wangu hata nitakapokuwa nimekwisha kupita; 23#Yn 1:18; 1 Tim 6:16; 1 Yoh 4:12nami nitaondoa mkono wangu, nawe utaniona nyuma yangu, bali uso wangu hautaonekana.

Iliyochaguliwa sasa

Kut 33: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia