Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kut 9:27-35

Kut 9:27-35 SUV

Farao akatuma watu, na kuwaita Musa na Haruni, na kuwaambia, Mimi nimekosa wakati huu; BWANA ni mwenye haki, na mimi na watu wangu tu waovu. Mwombeni BWANA; kwa kuwa zimekuwa za kutosha ngurumo hizo kuu na hii mvua ya mawe; nami nitawapa ninyi ruhusa mwende zenu, msikae zaidi. Musa akamwambia, Mara nitakapotoka mjini nitamwinulia BWANA mikono yangu; na hizo ngurumo zitakoma, wala haitanyesha mvua ya mawe tena; ili upate kujua ya kuwa dunia hii ni ya BWANA. Lakini, wewe na watumishi wako, najua ya kuwa ninyi hamtamcha BWANA Mungu bado. Kitani na shayiri zilipigwa; maana shayiri zilikuwa na masuke na kitani zilikuwa katika kutoa maua. Lakini ngano na kusemethu hazikupigwa; maana, zilikuwa hazijakua bado. Musa akatoka mjini, kutoka kwa Farao, akamwinulia BWANA mikono yake; na zile ngurumo na ile mvua ya mawe zikakoma, wala mvua haikunyesha juu ya nchi. Farao alipoona ya kwamba mvua na mvua ya mawe na ngurumo zimekoma, akazidi kufanya dhambi, na kuufanya moyo wake mzito, yeye na watumishi wake. Moyo wa Farao ukawa ni mgumu naye hakuwapa wana wa Israeli ruhusa waende zao; kama BWANA alivyonena kwa kinywa cha Musa.