Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwa 26

26
Isaka na Abimeleki
1 # Mwa 12:10; 20:2 Ikawa njaa katika nchi hiyo, mbali na njaa ile ya kwanza iliyokuwa siku za Ibrahimu. Isaka akamwendea Abimeleki, mfalme wa Wafilisti, huko Gerari. 2#Mwa 12:1; Zab 37:3BWANA akamtokea, akasema, Usishuke kwenda Misri, kaa katika nchi nitakayokuambia. 3#Mwa 22:16-18; Mwa 20:1; 28:15; Zab 39:12; Ebr 11:9; Mwa 12:2; 13:15; Zab 105:9Kaa ugenini katika nchi hiyo, nami nitakuwa pamoja nawe, na kukubariki, maana nitakupa wewe na uzao wako nchi hizi zote. Nami nitakifanya imara kiapo nilichomwapia Ibrahimu baba yako. 4#Zab 72:17Nitazidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, nami nitawapa uzao wako nchi hizi zote, na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia. 5#Mwa 22:16Kwa sababu Ibrahimu alisikia sauti yangu, akayahifadhi maagizo yangu, na amri zangu, na hukumu zangu, na sheria zangu. 6Isaka akakaa katika Gerari. 7#Mwa 12:13; 20:2; 24:16; Mit 29:25Watu wa mahali hapo wakamwuliza habari za mkewe. Akasema, Ni ndugu yangu huyu maana aliogopa kusema, Ni mke wangu, watu wa nchi wasije wakamwua kwa ajili ya Rebeka; kwa maana alikuwa mzuri wa uso. 8Ikawa alipokuwa amekaa huko siku nyingi, Abimeleki, mfalme wa Wafilisti, akachungulia dirishani, akamwona Isaka anacheza-cheza na Rebeka mkewe. 9Abimeleki akamwita Isaka, akasema, Yakini huyu ni mkeo, mbona ulisema, Ni ndugu yangu huyu? Isaka akamwambia, Kwa sababu nalisema, Nisife kwa ajili yake. 10#Mwa 20:9Abimeleki akasema, Ni nini hii uliyotutendea? Labda mtu mmojawapo angalilala na mkeo bila kufikiri, nawe ungalitutia hatiani. 11#Zab 105:15Basi Abimeleki akawaamuru watu wote, akisema, Amgusaye mtu huyu au mkewe lazima atauawa.
12 # Mt 13:8; Mk 4:8; Ayu 42:12; Mt 6:33 Isaka akapanda mbegu katika nchi ile, akapata mwaka ule vipimo mia kwa kimoja, BWANA akambariki. 13#Mit 10:22Na mtu huyu akawa mkuu, akazidi kusitawi, hata akawa mkuu sana. 14#Mwa 37:11; Mhu 4:4Akawa na mali ya kondoo, na mali ya ng’ombe, na watumwa wengi. Hao Wafilisti wakamhusudu. 15#Mwa 21:30Na vile visima vyote walivyochimba watumwa wa baba yake, siku za Ibrahimu babaye, Wafilisti walikuwa wamevifukia, wakavijaza kifusi. 16#Kut 1:9Abimeleki akamwambia Isaka, Utoke kwetu, maana wewe una nguvu sana kuliko sisi. 17Basi Isaka akatoka huko akapiga kambi katika bonde la Gerari, akakaa huko.
18 # Mwa 21:31 Isaka akarudi akavichimbua vile visima vya maji walivyovichimba siku za Ibrahimu babaye; maana wale Wafilisti walikuwa wamevifukia baada ya kufa kwake Ibrahimu; naye akaviita majina kufuata majina alivyoviita babaye. 19Watumwa wa Isaka wakachimba katika lile bonde, wakapata kisima cha maji yanayobubujika. 20#Mwa 21:25Wachungaji wa Gerari wakagombana na wachungaji wa Isaka wakisema, Maji haya ni yetu. Ndipo akakiita jina la kile kisima Eseki, kwa sababu waligombana naye. 21Wakachimba kisima kingine, wakagombania na hicho tena. Akakiita jina lake Sitna. 22#Mwa 17:6; Kut 1:7Akaondoka huko akachimba kisima kingine, wala hicho hawakukigombania. Akakiita jina lake Rehobothi, akasema, Kwa kuwa sasa BWANA ametufanyia nafasi, nasi tutazidi katika nchi. 23Akapanda kutoka hapo mpaka Beer-sheba.
24 # Mwa 15:1; 24:12; 26:3; Kut 3:6; Mdo 7:32; Rum 8:31 BWANA akamtokea usiku uleule, akasema, Mimi ni Mungu wa Ibrahimu baba yako, usiogope, maana mimi ni pamoja nawe, nami nitakubarikia, na kuzidisha uzao wako kwa ajili ya Ibrahimu mtumishi wangu. 25#Mwa 12:7; 13:18; Zab 116:17Akajenga madhabahu huko, akaliitia jina la BWANA. Akapiga hema yake huko, na watumwa wa Isaka wakachimba kisima huko.
26 # Mwa 21:22 Ndipo Abimeleki akamwendea kutoka Gerari, pamoja na Ahuzathi rafiki yake, na Fikoli, jemadari wa jeshi lake. 27#Amu 11:7Isaka akawauliza, Mbona mwanijia, nanyi mmenichukia, mkanifukuza kwenu? 28#Mwa 21:22,23Wakasema, Hakika tuliona ya kwamba BWANA alikuwa pamoja nawe; nasi tukasema, Na tuapiane, sisi na wewe, na kufanya mapatano nawe 29#Mwa 24:31; Zab 115:15ya kuwa hutatutenda mabaya, iwapo sisi hatukukugusa wewe, wala hatukukutendea ila mema, tukakuacha uende zako kwa amani; nawe sasa u mbarikiwa wa BWANA. 30#Mwa 19:3Basi akawafanyia karamu, nao wakala, wakanywa. 31#Mwa 21:31Wakaondoka asubuhi na mapema, wakaapiana wao kwa wao, kisha Isaka akawapa ruhusa, nao wakaenda zao kwa amani. 32Ikawa siku ileile, watumwa wa Isaka wakaja wakampasha habari za kile kisima walichokuwa wamekichimba, wakamwambia, Tumeona maji. 33#Mwa 21:31Naye akakiita jina lake Shiba; kwa hiyo jina la mji huo ni Beer-sheba, hata leo.
Esau na Wake Zake Wahiti
34 # Mwa 36:2 Esau alipokuwa mwenye miaka arobaini, akamwoa Yudithi, binti Beeri, Mhiti, na Basemathi, binti Eloni, Mhiti. 35#Mwa 27:46; 28:1,8Roho zao Isaka na Rebeka zikajaa uchungu kwa ajili yao.

Iliyochaguliwa sasa

Mwa 26: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia