Yer 29
29
Barua ya Yeremia kwa Mateka Waliokuwa Babeli
1 #
2 Fal 24:12-16; 2 Nya 36:10 Maneno haya ndiyo maneno ya waraka, ambao nabii Yeremia aliupeleka toka Yerusalemu, kwa hao waliobaki wa wakuu waliochukuliwa mateka, na kwa makuhani, na kwa manabii, na kwa watu wote, ambao Nebukadreza aliwachukua mateka toka Yerusalemu hata Babeli; 2(hapo walipokwisha kutoka Yerusalemu Yekonia mfalme, na mama yake mfalme, na matowashi, na wakuu wa Yuda na Yerusalemu, na mafundi, na wahunzi;) 3kwa mkono wa Elasa, mwana wa Shafani, na Gemaria, mwana wa Hilkia, (ambao Sedekia, mfalme wa Yuda, aliwatuma hata Babeli, kwa Nebukadreza, mfalme wa Babeli), kusema, 4BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, awaambia hivi watu wote waliochukuliwa mateka, niliowafanya wachukuliwe toka Yerusalemu mpaka Babeli; 5Jengeni nyumba, mkakae ndani yake, kapandeni bustani, mkale matunda yake; 6oeni wake, mkazae wana na binti; kawaozeni wake wana wenu, mkawaoze waume binti zenu, wazae wana na binti; mkaongezeke huko wala msipungue. 7#Dan 6:4; Rum 13:1,5; 1 Tim 2:1,2Kautakieni amani mji ule, ambao nimewafanya mchukuliwe mateka, mkauombee kwa BWANA; kwa maana katika amani yake mji huo ninyi mtapata amani. 8#Yer 14:14; 23:21; Efe 5:6Maana BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Manabii walio kati yenu, na wabashiri wenu, wasiwadanganye ninyi, wala msisikilize ndoto zenu, mnazootesha. 9Kwa maana kwa jina langu hutabiri maneno ya uongo kwenu; mimi sikuwatuma, asema BWANA. 10#2 Nya 36:21; Yer 25:11; Dan 9:2Maana BWANA asema hivi, Babeli utakapotimiziwa miaka sabini, nitawajilia ninyi, na kulitimiza neno langu jema kwenu, kwa kuwarudisha mahali hapa. 11Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho. 12#Dan 9:3Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza. 13#Law 26:39,40; Zab 32:6; Mt 7:7; Yer 24:7; Kum 4:29Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote. 14#Kum 4:7; Zab 32:6; Isa 55:6; Rum 10:20; Yer 23:3,8; 30:3Nami nitaonekana kwenu, asema BWANA, nami nitawarudisha watu wenu waliofungwa, nami nitawakusanya ninyi, nikiwatoa katika mataifa yote, na katika mahali pote, nilikowafukuza, asema BWANA; nami nitawaleta tena, hata mahali ambapo kutoka hapo naliwafanya mchukuliwe mateka. 15Maana mmesema, BWANA ametuinulia manabii huko Babeli. 16Maana BWANA asema hivi, katika habari za mfalme aketiye katika kiti cha enzi cha Daudi, na katika habari za watu wote wakaao ndani ya mji huu, ndugu zenu wasiokwenda pamoja nanyi kufungwa; 17#Yer 24:8-10BWANA wa majeshi asema hivi, Tazama, nitaleta juu yao upanga, na njaa, na tauni, nami nitawafanya kuwa kama tini mbovu, zisizoweza kuliwa, kwa kuwa ni mbovu sana. 18#Kum 29:21-28; 1 Fal 9:7,8; 2 Fal 25:8; Omb 2:15,16; Yer 15:4; 24:9Nami nitawafuatia kwa upanga, na njaa, na tauni, nami nitawatoa watupwe huko na huko katika falme zote za dunia, wawe kitu cha kulaaniwa, na cha kushangaza, na cha kuzomewa, na cha kulaumiwa, katika mataifa yote nilikowafukuza. 19#Yer 25:4; 32:33Kwa sababu hawakusikiliza maneno yangu, asema BWANA, ambayo naliwatuma watumishi wangu, hao manabii, nikiamka mapema, na kuwatuma; lakini hamkutaka kusikiliza, asema BWANA. 20#Amo 3:6; Mik 4:10Basi, lisikieni neno la BWANA, ninyi nyote mliochukuliwa mateka, niliowapeleka toka Yerusalemu mpaka Babeli.
21 #
2 Pet 2:1
BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, katika habari za Ahabu, mwana wa Kolaya, na katika habari za Sedekia, mwana wa Maaseya, wawatabiriao ninyi maneno ya uongo kwa jina langu; Tazama, nitawatia katika mikono ya Nebukadreza, mfalme wa Babeli, naye atawaua mbele ya macho yenu. 22#Mwa 48:20; Isa 65:15; Dan 3:6Tena katika habari zao laana itatumiwa na wafungwa wote wa Yuda, walioko Babeli, kusema, BWANA akufanye uwe kama Sedekia, na kama Ahabu, ambao mfalme wa Babeli aliwaoka motoni; 23#Sef 3:4; Mit 5:21; Yer 13:27; 16:17; Mal 3:5; Ebr 4:13kwa sababu wametenda upumbavu katika Israeli, nao wamezini na wake za jirani zao, nao wamenena maneno ya uongo kwa jina langu, nisiyowaamuru; nami ndimi nijuaye, nami ni shahidi, asema BWANA.
Barua kwa Shemaya
24Na katika habari za Shemaya, Mnehelami, utanena, ukisema, 25#2 Fal 25:18; Yer 21:1BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, ya kwamba, Kwa kuwa kwa jina lako mwenyewe umewapelekea barua watu wote walioko Yerusalemu, na Sefania, mwana wa Maaseya, kuhani, na makuhani wote, kusema, 26#Yer 20:1; Mdo 4:1; Kum 13:1-5; 2 Fal 9:11; Zek 13:3-6; 2 Nya 16:10; Yer 20:2; Mdo 16:24BWANA amekufanya kuhani badala ya Yehoyada, kuhani, ili mpate kuwa watumishi katika nyumba ya BWANA, kwa kila mtu aliye na wazimu, na kwa kila mtu ajifanyaye kuwa nabii, umtie katika mkatale na pingu. 27#Hes 16:3; Mdo 4:17Mbona, basi, hukumkemea Yeremia wa Anathothi, ajifanyaye kuwa nabii kwenu, 28ambaye ametuma watu kwetu katika Babeli, kusema, Uhamisho huu ni wa siku nyingi; jengeni nyumba, mkakae ndani yake; pandeni bustani, mkale matunda yake. 29Na Sefania, kuhani, akasoma barua hii masikioni mwa Yeremia nabii. 30Ndipo neno la BWANA likamjia Yeremia, kusema, 31#Yer 28:15Uwapelekee habari watu wote waliohamishwa, kusema, BWANA asema hivi, katika habari za Shemaya, Mnehelami; Kwa sababu Shemaya amewatabiria ninyi, lakini sikumtuma mimi, naye amewatumainisha neno la uongo; 32#Kut 20:5; Rum 2:8; Yer 28:16basi, BWANA asema hivi, Tazama, nitamwadhibu Shemaya, Mnehelami, na wazao wake; hatakuwa na mtu atakayekaa katika watu hawa, wala hatayaona mema nitakayowatendea watu wangu, asema BWANA; kwa sababu amenena maneno ya uasi juu ya BWANA.
Iliyochaguliwa sasa
Yer 29: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.