49
Hukumu dhidi ya Waamoni
1 #
Eze 21:28-32; 25:1-7; Amo 1:13-15; Sef 2:8-11 Habari za wana wa Amoni. BWANA asema hivi, Je, Israeli hana wana? Je! Hana mrithi? Basi, mbona Malkamu anamiliki Gadi, na watu wake wanakaa katika miji yake? 2#Amo 1:14Basi, kwa sababu hiyo, tazama, siku zinakuja, asema BWANA, nitakaposikizisha mshindo wa vita juu ya Raba, mji wa Amoni, nao utakuwa magofu ya ukiwa, na binti zake watateketezwa kwa moto; ndipo Israeli watawamiliki wao waliokuwa wakimmiliki, asema BWANA.
3 #
Isa 32:11; Yer 48:7 Piga yowe, Ee Heshboni,
Kwa maana Ai umeangamizwa;
Lieni, enyi binti za Raba,
Mjivike nguo za magunia;
Ombolezeni, mkipiga mbio
Huko na huko kati ya maboma;
Maana Malkamu atakwenda kuhamishwa,
Makuhani wake na wakuu wake pamoja.
4 #
Yer 21:13
Mbona unajisifu kwa sababu ya mabonde, bonde lako litiririkalo, Ee binti mwenye kuasi? Utumainiaye hazina zako, ukisema, Ni nani atakayenijilia? 5Tazama, nitaleta hofu juu yako, asema Bwana, BWANA wa majeshi, itakayotoka kwa wote wakuzungukao; nanyi mtafukuzwa nje, kila mtu mbali kabisa, wala hapana mtu wa kuwakusanya wapoteao. 6#Yer 48:47Lakini baada ya hayo nitawarudisha wana wa Amoni walio utumwani, asema BWANA.
Hukumu dhidi ya Edomu
7 #
Amo 1:11; Ayu 5:12-14; Oba 1:8; Isa 19:11 Habari za Edomu. BWANA wa majeshi asema hivi, Je! Hapana tena hekima katika Temani? Mashauri yamewapotea wenye busara? Je! Imetoweka hekima yao? 8#Isa 2:19; Yer 25:23Kimbieni, rudini nyuma, kaeni chini sana, enyi mnaokaa Dedani; maana nitaleta msiba wa Esau juu yake, wakati nitakapomwangalia. 9#Isa 17:6Je! Kama wachuma zabibu wangekujia, wasingeacha zabibu ziokotwe? Kama wangekujia wevi usiku, wasingeharibu hata watakapopata vya kutosha? 10#Isa 17:14Lakini nimemwacha Esau hana kitu, nimepafunua mahali pake pa siri, wala hataweza kujificha; kizazi chake kimeangamizwa, na ndugu zake, na jirani zake, naye mwenyewe hayuko. 11Waache watoto wako wasio na baba, mimi nitawahifadhi hai, na wajane wako na wanitumaini mimi. 12#Yer 25:29; Oba 1:16Maana BWANA asema hivi, Tazama, wale wasioandikiwa kunywea kikombe, watakinywea, ni hakika; na wewe je! U mtu ambaye hataadhibiwa kabisa? Hukosi utaadhibiwa, naam, kunywa utakunywa. 13#Mwa 22:16; Isa 45:23; 34:6; Amo 6:8; 1:12Kwa maana nimeapa kwa nafsi yangu, asema BWANA, kwamba Bozra utakuwa ajabu, na aibu, na ukiwa, na laana; na miji yake yote itakuwa ukiwa wa daima.
14 #
Oba 1:1,2 Nimepata habari kwa BWANA,
Na mjumbe ametumwa kati ya mataifa,
Akisema, Jikusanyeni, mkaujie,
Mkainuke kwenda vitani.
15Maana nimekufanya mdogo kati ya mataifa,
Na kudharauliwa katika watu.
16 #
Ayu 39:27; Mit 15:25; Amo 9:2 Katika habari za kuogofya kwako,
Kiburi cha moyo wako kimekudanganya,
Wewe ukaaye katika pango za majabali,
Ushikaye kilele cha milima;
Ujapofanya kioto chako juu sana kama tai,
Nitakushusha kutoka huko; asema BWANA.
17 #
Yer 18:16; 50:13 Na Edomu atakuwa ajabu; kila mtu apitaye atashangaa, na kuzomea, kwa sababu ya mapigo yake yote. 18#Mwa 19:24-25; Kum 29:23; Yer 50:40; Amo 4:11Kama vile vilivyotokea wakati wa kuangushwa Sodoma na Gomora, na miji iliyokuwa karibu nayo, asema BWANA; hapana mtu atakayekaa huko, wala hapana mwanadamu atakayekaa huko kama mgeni akaavyo. 19#Yer 4:17; 12:5; Zek 11:3; Kut 15:11; Zab 89:6-8; Ayu 41:10Angalia, atapanda kama simba toka kiburi cha Yordani juu ya malisho yasiyonyauka; lakini nitamkimbiza ghafula ayaache; na yeye aliye mteule nitamweka juu yake; maana ni nani aliye kama mimi? Tena ni nani atakayeniandikia muda? Tena ni mchungaji yupi atakayesimama mbele zangu?
20 #
Yer 50:45
Basi, lisikieni shauri la BWANA;
Alilolifanya juu ya Edomu;
Na makusudi yake aliyoyakusudia
Juu yao wakaao Temani;
Hakika watawaburura, naam, wadogo wa kundi;
Hakika malisho yao yatafadhaika kwa ajili yao.
21Nchi yatetemeka kwa sauti ya kuanguka kwao;
Kuna kilio, sauti yake yasikiwa katika Bahari ya Shamu.
22 #
Yer 4:13
Tazama, atapanda na kuruka kama tai, na kutandaza mabawa yake juu ya Bozra; na mioyo ya mashujaa wa Edomu siku hiyo itakuwa kama moyo wa mwanamke katika utungu wake.
Hukumu dhidi ya Dameski
23 #
Isa 17:1-3; Amo 1:3-5; Zek 9:1 Habari za Dameski.
Hamathi umetahayarika, na Arpadi pia;
Maana wamesikia habari mbaya;
Wameyeyuka kabisa;
Huzuni iko baharini, haiwezi kutulia.
24 #
Isa 13:8
Dameski umedhoofika;
Umejigeuza kukimbia; tetemko limeushika;
Dhiki na huzuni zimeupata,
Kama za mwanamke katika utungu wake.
25 #
Yer 51:41
Imekuwaje mji wa sifa haukuachwa, mji wa furaha yangu? 26Kwa hiyo vijana wake wataanguka katika njia kuu zake, na watu wote wa vita watanyamazishwa katika siku hiyo, asema BWANA wa majeshi. 27#Amo 1:4; 2 Fal 13:3Nami nitawasha moto katika ukuta wa Dameski, nao utayateketeza majumba ya Ben-hadadi.
Hukumu dhidi ya Kedari na Hazori
28 #
Ayu 1:3
Habari za Kedari, na za falme za Hazori, ambazo Nebukadreza, mfalme wa Babeli, alizipiga. BWANA asema hivi, Ondokeni, pandeni hata Kedari, mkawateke nyara wana wa mashariki. 29#Zab 120:5Hema zao na makundi yao watayatwaa; watachukulia mbali mapazia yao kwa faida yao wenyewe, na vyombo vyao vyote, na ngamia zao; nao watawapigia kelele wakisema, Hofu ziko pande zote. 30Kimbieni ninyi, enendeni mbali mkitanga-tanga, kaeni chini sana, enyi mkaao Hazori, asema BWANA; maana Nebukadreza, mfalme wa Babeli, amefanya shauri juu yenu, naye amekusudia neno juu yenu. 31#Hes 23:9; Kum 33:28; Amu 18:28; Mik 7:14Ondokeni, pandeni hata taifa lililo katika hali ya raha, likaalo bila kuhangaika, asema BWANA; wasio na malango wala makomeo, wakaao peke yao. 32#Kum 28:64; Eze 5:10; Yer 25:23Na ngamia zao watakuwa mateka, na wingi wa makundi yao utakuwa nyara; nami nitawatawanya hata pepo zote watu wale wanyoao denge; nami nitaleta msiba wao toka pande zao zote, asema BWANA. 33#Yer 9:11; Mal 1:3Na Hazori utakuwa kao la mbwa-mwitu; ukiwa milele; hapana mtu atakayekaa huko, wala hapana mwanadamu atakayekaa huko kama mgeni akaavyo.
Hukumu dhidi ya Elamu
34 #
Mwa 10:22; Yer 25:25 Neno la BWANA lililomjia Yeremia, nabii, juu ya Elamu, mwanzo wa kumiliki kwake Sedekia, mfalme wa Yuda, kusema, 35#Mwa 14:1; Ezr 4:9; Isa 21:2; Dan 8:2BWANA wa majeshi asema hivi, Tazama nitauvunja upinde wa Elamu, ulio mkuu katika nguvu zao. 36Na juu ya Elamu nitazileta pepo nne, toka pembe nne za mbinguni, nami nitawatawanya hata pepo nne zote, wala hapana taifa ambalo hawatalifikilia watu wa Elamu waliofukuzwa. 37#Yer 48:2Nami nitawafadhaisha watu wa Elamu mbele ya adui zao, na mbele ya hao wanaowatafuta roho zao; nami nitawaletea mabaya, naam, hasira yangu kali, asema BWANA; nami nitautuma upanga uwafuatie, hata nitakapowaangamiza; 38#Yer 43:10; Dan 7:9nami nitaweka kiti changu cha enzi huko Elamu, nami nitawaharibu, mfalme na wakuu, watoke huko, asema BWANA. 39Lakini itakuwa, katika siku za mwisho, nitawarudisha wafungwa wa Elamu, asema BWANA.