5
Uovu mwingi wa Watu wa Mungu
1 #
Eze 22:30; Mik 7:2; Zab 12:1 Pigeni mbio huku na huku katika njia za Yerusalemu, mkaone sasa, na kujua, na kutafuta katika viwanja vyake, kwamba mwaweza kumpata mtu mmoja, kwamba yuko mtu mmoja awaye yote atendaye kwa haki, atafutaye uaminifu; nami nitausamehe mji huo. 2#Tit 1:16Na wajaposema, Kama BWANA aishivyo, hakika waapa kwa uongo. 3#2 Nya 16:9; Isa 1:5; Yer 7:28; Sef 3:2Ee BWANA, macho yako je! Hayaangalii uaminifu? Umewapiga, lakini hawakuhuzunika; umewakomesha, lakini wamekataa kurudiwa wamefanya nyuso zao kuwa ngumu kuliko mwamba wamekataa kurudi. 4#Yer 8:7Ndipo nikasema, Hakika, hawa ni maskini; ni wajinga hawa; maana hawaijui njia ya BWANA, wala hukumu ya Mungu wao; 5#Mik 3:1; Zab 2:3nitawaendea watu wakubwa, nami nitasema nao; kwa maana hao wanaijua njia ya BWANA, na hukumu ya Mungu wao. Bali hawa kwa nia moja wameivunja nira, na kuvikata vifungo. 6#Yer 4:7; Hab 1:8; Hos 13:7Basi, kwa hiyo, simba atokaye mwituni atawaua, mbwa-mwitu wa jioni atawateka, chui ataivizia miji yao, kila mtu atokaye humo atararuliwa vipande vipande; kwa sababu makosa yao ni mengi, na kurudi nyuma kwao kumezidi. 7#Yos 23:7; Yer 12:16; Amo 8:14; Gal 4:8; Kum 32:15Nawezaje kukusamehe? Watoto wako wameniacha mimi, na kuapa kwa hao ambao si miungu; nilipokuwa nimewashibisha chakula, walizini, wakakutana wengi pamoja katika nyumba za makahaba. 8#Eze 22:11; 2 Sam 11:2-4; Yer 13:27Walikuwa kama farasi walioshiba wakati wa asubuhi; kila mmoja akalia kwa kutamani mke wa mwenzake. 9#Isa 1:24; Yer 44:22; Eze 7:9Je! Nisiwapatilize kwa sababu ya mambo hayo? Asema BWANA; na nafsi yangu, je! Nisijilipize kisasi juu ya taifa la namna hii?
10 #
Yer 39:8
Pandeni juu ya kuta zake mkaharibu, lakini msiharibu kabisa; ondoeni matawi yake; kwa maana si yake BWANA. 11#Yer 3:20Maana nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda wamenitenda kwa hiana sana, asema BWANA. 12#2 Nya 36:16; Isa 28:15; Yer 14:13Wamemkataa BWANA, na kusema, Si yeye; wala hayatatupata mabaya; wala hatutaona upanga wala njaa; 13na manabii watakuwa upepo, wala neno lake halimo ndani yao; basi ndivyo watakavyotendwa. 14#Yer 1:9; Hos 6:5; Ufu 11:5Kwa sababu hiyo BWANA, Mungu wa majeshi, asema hivi, Kwa sababu mnasema neno hili, tazama, nitafanya maneno yangu katika kinywa chako kuwa moto, na watu hawa kuwa kuni, nao moto utawala. 15#Kum 28:49; Isa 5:26; Yer 1:15; Isa 39:3Angalia, nitaleta taifa juu yenu litokalo mbali sana, Ee nyumba ya Israeli, asema BWANA; ni taifa hodari, ni taifa la zamani sana, taifa ambalo hujui lugha yake, wala huyafahamu wasemayo. 16Podo lao ni kaburi wazi, ni mashujaa wote pia. 17#Law 26:16; Kum 28:31; Amu 6:3,4Nao watakula mavuno yako, na mkate wako, ambao iliwapasa wana wako na binti zako kuula; watakula makundi yako ya kondoo na ya ng’ombe; watakula mizabibu yako na mitini yako; wataiharibu miji yako yenye boma, uliyokuwa ukiitumainia, naam, wataiharibu kwa upanga. 18Lakini hata katika siku zile, asema BWANA, sitawakomesha ninyi kabisa. 19#Kum 29:24; 28:48; 1 Fal 9:8; Yer 13:22Tena itakuwa mtakapouliza, BWANA ametutenda mambo hayo yote kwa sababu gani? Ndipo utakapowaambia, Vile vile kama ninyi mlivyoniacha mimi, na kuwatumikia miungu mingine katika nchi yenu wenyewe, ndivyo mtakavyowatumikia wageni katika nchi isiyo yenu.
20Tangazeni neno hili katika nyumba ya Yakobo, litangazeni katika Yuda, kusema, 21#Isa 6:9-10; Eze 12:2; Mk 8:18; Mt 13:14; Yn 12:40; Mdo 28:26Sikilizeni neno hili, enyi watu wajinga msio na ufahamu; mlio na macho ila hamwoni; mlio na masikio ila hamsikii. 22#Ufu 15:4; Ayu 26:10; Mit 8:29; Ayu 38:8-11Je! Hamniogopi mimi? Asema BWANA; hamtatetemeka mbele za uso wangu; mimi niliyeweka mchanga kuwa mpaka wa bahari, kwa amri ya daima, isiweze kuupita? Mawimbi yake yajapoumuka-umuka, hayawezi kushinda nguvu; yajapovuma sana, hayawezi kuupita. 23Lakini watu hawa wana moyo wa kuasi na ukaidi; wameasi, wamekwenda zao. 24#Mt 5:45; Yoe 2:23; Mwa 8:22Wala hawasemi mioyoni mwao, Basi, na tumche BWANA, Mungu wetu, aletaye mvua, mvua ya mwaka, na mvua ya vuli, kwa wakati wake; na kutuwekea juma za mavuno zilizoamriwa. 25Maovu yenu yameyageuza haya, na dhambi zenu zimewazuilia mema msiyapate. 26Maana katika watu wangu wameonekana watu waovu; huotea kama vile watu wategao mitego; hutega mtego, na kunasa watu. 27Kama tundu lijaavyo ndege, kadhalika nyumba zao zimejaa hila; kwa hiyo wamekuwa wakuu, wamepata mali. 28#Zab 73:12Wamewanda sana, wang’aa; naam, wamepita kiasi kwa matendo maovu; hawatetei madai ya yatima, ili wapate kufanikiwa; wala hawaamui haki ya mhitaji. 29#Mal 3:5Je! Nisiwapatilize kwa mambo hayo? Asema BWANA; na nafsi yangu, je! Nisijilipize kisasi juu ya taifa la namna hii?
30Jambo la ajabu, la kuchukiza, limetokea katika nchi hii! 31#Eze 13:6; Isa 30:10Manabii wanatabiri uongo, na makuhani wanatawala kwa msaada wa hao; na watu wangu wanapenda mambo yawe hivyo. Nanyi mtafanya nini mwisho wake?