15
Elifazi Anena: Ayubu Anapuuza Dini
1Ndipo Elifazi, Mtemani, akajibu, na kusema,
2Je! Yapasa mtu mwenye hekima kujibu kwa ujuzi wa uvuvio,
Na kujaza tumbo lake na upepo wa mashariki?
3Je! Ahoji na mazungumzo yasiyo faida,
Au kwa maneno ambayo hawezi kufanya mema kwayo?
4Naam, wewe waondoa kicho,
Nawe wazuia ibada mbele za Mungu.
5Kwani uovu wako unakufundisha kinywa chako,
Nawe wachagua ulimi wake mwenye hila.
6Kinywa chako mwenyewe chakuhukumia makosa, wala si mimi;
Naam, midomo yako mwenyewe hushuhudia juu yako.
7 #
Mit 8:25
Je! Wewe u mtu wa kwanza aliyezaliwa?
Au, ulizawa wewe kabla ya milima?
8 #
Mt 11:25; Rum 11:34; 1 Kor 2:11 Je! Umesikia mashauri ya siri ya Mungu?
Nawe je! Wazuia hekima iwe yako tu?
9 #
Ayu 13:2
Je! Wewe wajua neno lipi, ambalo sisi hatulijui?
Nawe wafahamu nini, ambalo halimo ndani yetu?
10 #
Kum 32:7; Ayu 8:8-10; Mit 16:31 Wenye mvi, na walio wazee sana, wote wapo pamoja nasi,
Ambao ni wazee kuliko baba yako.
11Je! Utulizi wa Mungu ni mdogo sana kwako,
Na hilo neno la upole si kitu kwako?
12Mbona moyo wako unakutaharakisha!
Na macho yako, je! Kwani kung’ariza?
13Hata ukageuza roho yako iwe kinyume cha Mungu,
Na kuyatoa maneno kama hayo kinywani mwako.
14 #
Ayu 25:4-6; 14:4; Zab 14:3; Mit 20:9; Mhu 7:20; Rum 7:18; Efe 2:2,3 Je! Mwanadamu ni kitu gani, hata akawa safi?
Huyo aliyezaliwa na mwanamke, hata awe na haki?
15 #
Ayu 25:5
Yeye hawategemei watakatifu wake;
Naam, mbingu nazo si safi machoni pake.
16 #
Zab 14:3; Mit 19:28 Sembuse mtu ambaye ni mwenye kuchukiza na uchafu,
Mwanadamu anywaye uovu kama anywavyo maji!
17Mimi nitakuonyesha, unisikilize;
Na hayo yote niliyoyaona nitayanena;
18 #
Mwa 18:19
(Ambayo watu wenye hekima wameyatangaza
Tokea baba zao, wala hawakuyaficha;
19 #
Yoe 3:17
Waliopewa hiyo nchi peke yao,
Wala mgeni hakupita kati yao);
20 #
Zab 90:12
Mtu mwovu huwa na uchungu siku zake zote,
Hata hesabu ya miaka aliyowekewa mwenye kuonea.
21 #
1 The 5:3
Sauti za utisho zi masikioni mwake;
Katika kufanikiwa kwake mtekaji nyara atamjia juu yake;
22Yeye hasadiki kwamba atarudi kutoka gizani,
Naye hungojewa na upanga;
23 #
Zab 59:15; Ayu 18:12 Hutanga-tanga ili apate chakula, akisema, Ki wapi?
Ajua kwamba siku ya giza i tayari karibu yake;
24Mateso na dhiki humtia hofu;
Humshinda kama vile mfalme aliye tayari kwa vita;
25 #
Mal 3:13
Kwa kuwa amenyosha mkono wake juu ya Mungu,
Na kuendelea kwa kiburi kinyume cha Mwenyezi;
26Humshambulia na shingo ngumu,
Kwa mafundo makubwa ya ngao zake;
27 #
Zab 17:10
Kwa kuwa amefunika uso wake na kunona kwake,
Na kuwandisha mafuta kiunoni mwake;
Naye amekaa katika miji iliyo ukiwa,
28Katika nyumba ambazo hapana mtu azikaaye,
Zilizokuwa tayari kuwa magofu.
29Hatakuwa tajiri, wala mali zake hazitadumu,
Wala maongeo yao hayatainama nchi.
30 #
Ayu 4:9; Isa 11:4; Ufu 19:15 Hataondoka gizani;
Ndimi za moto zitayakausha matawi yake,
Naye ataondoka kwa pumzi za kinywa chake.
31 #
Zab 62:10; Isa 59:4 Asiutumainie ubatili, na kujidanganya;
Kwa kuwa huo ubatili ndio utakaokuwa ujira wake.
32 #
Ayu 22:16; Zab 55:23 Jambo hili litatendeka kabla ya wakati wake,
Na tawi lake halitasitawi.
33Atayapukutisha mapooza yake kama mzabibu,
Na kuyatupa maua yake kama mzeituni.
34 #
Isa 33:14
Kwa kuwa jamii ya hao wasiomcha Mungu watakuwa tasa,
Na moto utateketeza mahema yenye rushwa.
35 #
Zab 7:14; Isa 59:4 Wao hutunga mimba ya madhara, na kuzaa uovu,
Nalo tumbo lao hutengeza udanganyifu.