Ayu 18
18
Bildadi Anena: Mungu Huwaadhibu Waovu
1Ndipo Bildadi, Mshuhi, akajibu, na kusema,
2Je! Hata lini utayategea maneno mitambo?
Fikiri, kisha baadaye tutanena.
3 #
Ayu 12:7; Zab 73:22 Twahesabiwa kuwa wanyama kwa sababu gani,
Tena kuwa wanajisi machoni pako?
4 #
Ayu 13:14
Wewe ujiraruaye mwenyewe katika hasira yako,
Je! Dunia itaachwa kwa ajili yako wewe?
Au jabali litaondolewa mahali pake?
5 #
Ayu 21:17; Mit 13:9 Naam, mwanga wa waovu utazimika,
Wala mwali wa moto wake hautang’aa.
6Mwanga hemani mwake utakuwa giza,
Nayo taa iliyo juu yake itazimishwa.
7Hatua zake za nguvu zitasongwa,
Na shauri lake mwenyewe litamwangusha chini.
8Kwani ametupwa katika wavu na miguu yake mwenyewe,
Naye huenda juu ya matanzi.
9Tanzi litamshika kisigino chake,
Na mtambo utamgwia.
10Amefichiwa tanzi chini,
Na mtego amewekewa njiani.
11 #
Ayu 6:4; Zab 73:19; Yer 6:25; 2 Kor 5:11 Matisho yatamtia hofu pande zote,
Na kumfukuza karibu na visigino vyake.
12 #
Ayu 15:23; 1 The 5:3 Nguvu zake zitaliwa na njaa,
Na msiba utakuwa tayari kwa kusita kwake.
13Utakula via vya mwili wake,
Naam, mzaliwa wa kwanza wa mauti atavila via vyake.
14 #
Ayu 8:14; Zab 112:10; Mit 10:28; Mt 7:26,27 Atang’olewa katika hema yake aliyokuwa akiitumaini;
Naye atapelekwa kwake mfalme wa utisho.
15 #
Mwa 19:24
Ambacho si chake kitakaa katika hema yake;
Kiberiti kitamwagwa juu ya makazi yake.
16Chini, mizizi yake itakaushwa;
Na juu, tawi lake litasinyaa.
17 #
Zab 34:16; Mit 2:22 Kumbukumbu lake litakoma katika nchi,
Wala hatakuwa na jina mashambani.
18Atakimbizwa kutoka mwangani hata gizani,
Na kufukuzwa atoke duniani.
19 #
Isa 14:22; Yer 22:30 Hatakuwa na mwana wala mjukuu kati ya watu wake,
Wala hatasalia mtu hapo alipokaa.
20Hao wanaokaa magharibi watastaajabia siku yake,
Kama vile wanaokaa mashariki walivyotiwa hofu.
21 #
Yer 9:3; 1 The 4:5; 2 The 1:8; Tit 1:16 Hakika ndivyo yalivyo makazi ya wapotovu,
Na hapa ni mahali pake asiyemjua Mungu.
Iliyochaguliwa sasa
Ayu 18: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.