24
Ayubu Alalamikia Udhalimu Duniani
1 #
Mdo 1:7
Mbona nyakati zisiwekwe na Mwenyezi?
Na hao wamjuao mbona hawazioni siku zake?
2 #
Kum 19:14
Wako waziondoao alama za mipaka;
Huyachukua makundi kwa jeuri na kuyalisha.
3 #
Kum 24:6,10,12,17 Humfukuza punda wake asiye baba,
Humtwaa rehani ng’ombe wake mwanamke mjane.
4 #
Mit 28:28
Humgeuza mhitaji aiache njia;
Maskini wa nchi hujificha pamoja.
5Tazama, kama punda-mwitu jangwani
Wao hutoka kwenda kazini mwao, wakitafuta chakula kwa bidii;
Jangwa huwapa chakula cha watoto wao.
6Hukata nafaka zao mashambani;
Na kuokota zabibu za waovu.
7 #
Kut 22:26; Kum 24:12; Isa 58:7 Hujilaza usiku kucha uchi pasipo nguo,
Wala hawana cha kujifunika baridi.
8 #
Omb 4:5
Hutota kwa manyunyo ya milimani,
Na kuambatana na jabali kwa kukosa sitara,
9Wako wamwondoao matitini kwa nguvu huyo asiye na baba,
Na kutwaa rehani kwa maskini;
10Hata wazunguke uchi pasipo mavazi,
Nao wakiwa na njaa huchukua miganda;
11Hushindika mafuta ndani ya makuta ya watu hao;
Wakanyaga mashinikizo, nao wana kiu.
12 #
Mhu 8:11
Watu huugua toka mji ulio na watu wengi,
Na roho yake aliyejeruhiwa hupiga ukelele;
Wala Mungu hauangalii upumbavu.
13Hawa ni katika hao waliouasi mwanga;
Hawazijui njia zake,
Wala hawakai katika mapito yake.
14Mwuaji huamka asubuhi kukipambauka, huwaua maskini na wahitaji;
Tena wakati wa usiku yu kama mwivi.
15Tena jicho lake mzinifu hungojea wakati wa giza-giza,
Akisema, Hapana jicho litakaloniona;
Naye huuficha uso wake.
16 #
Yn 3:20
Wao hutoboa nyumba gizani;
Hujifungia ndani wakati wa mchana;
Hawaujui mwanga.
17Kwani asubuhi kwao wote ni kama giza tupu;
Kwani wao wavijua vitisho vya hiyo giza tupu.
18Mwasema, Yeye ni mwepesi juu ya uso wa gharika;
Sehemu yao inalaaniwa duniani;
Hageuki kwenda njia ya mizabibuni.
19Chaka na hari hukausha maji ya theluji;
Kuzimu nako hao ambao wamefanya dhambi.
20 #
Mit 10:7
Tumbo lililomzaa litamsahau; buu litamla na kuona tamu;
Hatakumbukwa tena;
Na udhalimu utavunjwa kama mti.
21Naam, yeye huwala walio tasa wasiozaa;
Wala hamtendei mema mwanamke mjane.
22Lakini Mungu huwadumisha wenye uwezo kwa nguvu zake;
Huinuka, wasiokuwa na tumaini la kuishi.
23Huwapa kuwa na salama, nao wapumzika kwayo;
Na macho yake ya juu ya njia zao.
24 #
Zab 37:35,36 Wao wametukuzwa; lakini kitambo kidogo hutoweka;
Naam, hushushwa, na kuondolewa njiani kama wengine wote,
Nao hukatwa kama vile masuke ya ngano.
25Na kama sivyo sasa, ni nani atakayenihukumu kuwa ni mwongo,
Na kuyafanya maneno yangu kuwa si kitu?