Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ayu 33

33
Elihu Amkemea Ayubu
1 # Ayu 13:6 Walakini, Ayubu, nakuomba usikilize matamko yangu,
Ukayasikilize maneno yangu yote.
2Tazama basi, nimefunua kinywa changu,
Ulimi wangu umenena kinywani mwangu.
3 # 1 The 1:3 Maneno yangu yatatamka uelekevu wa moyo wangu;
Na hayo niyajuayo midomo yangu itayanena kwa unyofu.
4 # Mwa 2:7 Roho ya Mungu imeniumba,
Na pumzi za Mwenyezi hunipa uhai.
5Kwamba waweza, nijibu;
Yapange maneno yako sawasawa mbele yangu, usimame.
6 # Ayu 9:32 Tazama, mimi ni mbele ya Mungu kama ulivyo wewe;
Mimi nami nilifinyangwa katika udongo.
7 # Ayu 13:21 Tazama, utisho wangu hautakutia hofu wewe,
Wala sitakulemea kwa uzito.
8Hakika umenena masikioni mwangu,
Nami nimesikia sauti ya maneno yako, ukisema,
9 # Ayu 10:7 Mimi ni safi, sina makosa;
Sina hatia, wala hapana uovu ndani yangu;
10 # Ayu 13:24 Tazama, yuaona sababu za kufarakana nami,
Hunihesabu kuwa ni adui yake;
11 # Ayu 13:27 Hunitia miguu yangu katika mkatale,
Na mapito yangu yote huyapeleleza.
12 # Mhu 7:20 Tazama, nitakujibu, katika neno hili huna haki;
Kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mwanadamu.
13 # Isa 45:9 Nawe kwani kumnung’unikia,
Kwa vile asivyotoa hesabu ya mambo yake yote?
14Kwa kuwa Mungu hunena mara moja,
Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali.
15 # Ayu 4:13 Katika ndoto, katika maono ya usiku,
Usingizi mzito uwajiliapo watu,
Katika usingizi kitandani;
16Ndipo huyafunua masikio ya watu,
Na kuyatia muhuri mafundisho yao,
17Ili amwondoe mtu katika makusudio yake,
Na kumfichia mtu kiburi;
18Yeye huizuia nafsi yake isiende shimoni,
Na uhai wake usiangamie kwa upanga.
19 # Kum 8:5; Zab 94:12,13 Yeye hutiwa adabu kwa maumivu kitandani mwake,
Na kwa mashindano yaendeleayo daima mifupani mwake;
20Hata roho yake huchukia chakula,
Na nafsi yake huchukia nyama nzuri.
21 # Zab 102:5 Nyama ya mwili wake huliwa, isionekane;
Na mifupa yake isiyoonekana yatokea nje.
22Naam, nafsi yake inakaribia shimoni,
Na uhai wake unakaribia waangamizi.
23 # 2 Nya 36:15,16; Mal 2:7 Kwamba akiwapo malaika pamoja naye,
Mkalimani, mmoja katika elfu,
Ili kumwonyesha binadamu hayo yampasayo;
24 # Rum 3:24 Ndipo amwoneapo rehema, na kusema,
Mwokoe asishuke shimoni;
Mimi nimeuona ukombozi.
25Nyama ya mwili wake itakuwa laini kuliko ya mtoto;
Huzirudia siku za ujana wake;
26 # 2 Fal 20:2-5; Zab 6:1-9 Yeye humwomba Mungu, naye akamtakabalia;
Hata auone uso wake kwa furaha;
Naye humrejezea mtu haki yake.
27Yeye huimba mbele ya watu, na kusema,
Mimi nimefanya dhambi, na kuyapotosha hayo yaliyoelekea,
Wala sikulipizwa jambo hilo;
28Yeye ameikomboa nafsi yangu isiende shimoni,
Na uhai wangu utautazama mwanga.
29Tazama, hayo yote ni Mungu anayeyafanya,
Mara mbili, naam, hata mara tatu, kwa mtu,
30 # Zab 40:2; Zek 9:11 Ili kurudisha roho yake itoke shimoni,
Ili atiwe mwanga kwa mwanga wa walio hai.
31Angalia sana, Ee Ayubu, unisikilize;
Nyamaza, mimi nitasema.
32 # 2 Kor 1:24 Kama una neno la kusema, nijibu;
Nena, kwani nataka kukuhesabia kuwa na haki.
33 # Zab 34:11 Kama sivyo, unisikilize mimi;
Nyamaza, nami nitakufunza hekima.

Iliyochaguliwa sasa

Ayu 33: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia