Ayu 35
35
Elihu Alaani Haki ya Kibinafsi
1Tena Elihu akajibu na kusema,
2Je! Wewe wadhani kwamba haya ni haki yako,
Au je! Wasema, Haki yangu ni zaidi kuliko ya Mungu,
3Maana wasema, Kutakuwa na faida gani kwako wewe?
Tena, Nitapata faida gani, kuliko nikifanya dhambi?
4Mimi nitakujibu,
Na hawa wenzio pamoja nawe.
5Ziangalie mbingu ukaone;
Na mawingu yaangalie, yaliyo juu kuliko wewe.
6 #
Ayu 22:2-3
Ikiwa umefanya dhambi, umefanya nini juu yake?
Yakiwa makosa yako yameongezeka, wamfanyia nini yeye?
7 #
Mit 9:12; Rum 11:35 Ikiwa u mwenye haki, wampa kitu gani?
Au yeye hupokea nini mkononi mwako?
8Uovu wako waweza kumwumiza mtu kama wewe;
Na haki yako yaweza kumfaa mwanadamu.
9 #
Kut 2:23; Neh 5:5; Ayu 24:12; Zab 12:5; Lk 18:3-7 Kwa sababu ya wingi wa jeuri wao hulia;
Walilia msaada kwa sababu ya mkono wa wakuu.
10 #
Mhu 12:1; Isa 51:13; 1 Pet 4:19; Zab 42:8; Mdo 16:25 Wala hapana asemaye, Yuko wapi Mungu Muumba wangu,
Awapaye nyimbo wakati wa usiku;
11 #
Ayu 32:8; Zab 8:6; 1 Yoh 5:20 Atufundishaye zaidi ya hayawani wa nchi,
Na kutufanya wenye hekima kuliko ndege za angani?
12 #
Mit 1:28
Hulia huko, lakini hapana ajibuye,
Kwa sababu ya kiburi cha watu waovu.
13Hakika Mungu hatasikia ubatili,
Wala Mwenyezi hatauangalia.
14Sembuse usemapo wewe ya kuwa humwangalii,
Hiyo daawa i mbele yake, nawe wamngojea!
15Lakini sasa, kwa sababu yeye hakukujilia katika hasira zake,
Wala hauangalii sana unyeti;
16 #
Ayu 34:35,37 Ndiposa Ayubu hufunua kinywa chake kwa ubatili;
Huongeza maneno pasipo maarifa.
Iliyochaguliwa sasa
Ayu 35: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.