12
Wafalme Walioshindwa na Musa
1 #
Hes 21:21-35; Kum 2:26—3:11; Amu 11:18; Isa 16:2; Kum 3:8,9 Basi hawa ndio wafalme wa nchi, ambao wana wa Israeli waliwapiga na kuimiliki nchi yao ng’ambo ya pili ya Yordani, upande wa maawio ya jua, kutoka bonde la Amoni mpaka mlima wa Hermoni, na nchi yote ya Araba upande wa mashariki; 2Sihoni mfalme wa Waamori, aliyekaa huko Heshboni, naye ndiye aliyetawala toka Aroeri, ulioko kando ya bonde la Arnoni, na toka huo mji ulio katikati ya bonde, na nusu ya Gileadi, hata kuufikilia mto wa Yaboki, mpaka wa hao wana wa Amoni; 3#Kum 3:17; Yos 13:20na nchi ya Araba mpaka bahari ya Kinerethi, kuelekea mashariki, tena mpaka bahari ya Ataba, mpaka Bahari ya Chumvi, kwendea mashariki, njia ya kwendea Beth-yeshimothi; tena upande wa kusini, chini ya matelemko ya Pisga; 4#Hes 21:35; Kum 3:11tena mpaka wa Ogu mfalme wa Bashani, aliyekuwa wa hayo mabaki ya hao Warefai, aliyekaa Ashtarothi na Edrei, 5#Yos 13:11; Kum 3:14; 1 Sam 27:8; 2 Sam 3:3; 13:37; 2 Fal 25:23naye alitawala katika mlima wa Hermoni, na katika Saleka, na katika Bashani yote, hata mpaka wa Wageshuri, na Wamaaka, na nusu ya Gileadi, mpaka wa huyo Sihoni mfalme wa Heshboni. 6#Hes 32:33; Kum 3:12Musa mtumishi wa BWANA na wana wa Israeli wakawapiga; naye Musa mtumishi wa BWANA akawapa Wareubeni, na Wagadi, na nusu ya kabila ya Manase iwe urithi wao.
7 #
Mwa 14:6; 32:3 Hawa ni wafalme wa hiyo nchi ambao Yoshua na wana wa Israeli waliwapiga ng’ambo ya pili ya Yordani upande wa magharibi, kutoka Baal-gadi katika bonde la Lebanoni mpaka kilima cha Halaki, kilichoelekea Seiri; Yoshua naye akawapa kabila za Israeli iwe milki yao sawasawa na magawanyo yao; 8#Kut 3:8; Yos 10:40katika nchi ya vilima, na katika Shefela, na katika nchi ya Araba, na katika matelemko, na katika bara, na katika Negebu; nchi ya Mhiti, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi; 9#Yos 6:2; 8:29mfalme wa Yeriko, mmoja; mfalme wa Ai, ulio karibu na Betheli, mmoja; 10#Yos 10:23mfalme wa Yerusalemu, mmoja; mfalme wa Hebroni, mmoja; 11mfalme wa Yarmuthi, mmoja; na mfalme wa Lakishi, mmoja; 12mfalme wa Egloni, mmoja; na mfalme wa Gezeri, mmoja; 13mfalme wa Debiri, mmoja; na mfalme wa Gederi, mmoja; 14mfalme wa Horma, mmoja; na mfalme wa Aradi, mmoja; 15mfalme wa Libna, mmoja; na mfalme wa Adulamu, mmoja; 16mfalme wa Makeda, mmoja; na mfalme wa Betheli, mmoja; 17#Yos 19:13; 1 Fal 4:10mfalme wa Tapua, mmoja; na mfalme wa Heferi, mmoja; 18#Isa 33:9mfalme wa Afeka, mmoja; na mfalme wa Lasharoni, mmoja; 19mfalme wa Madoni, mmoja; na mfalme wa Hazori, mmoja; 20#Yos 11:1; 19:15mfalme wa Shimron-meroni, mmoja; na mfalme wa Akshafu, mmoja; 21mfalme wa Taanaki, mmoja; na mfalme wa Megido, mmoja; 22#Yos 19:37na mfalme wa Kedeshi, mmoja; mfalme wa Yokneamu wa Karmeli, mmoja; 23#Mwa 14:1,2; Isa 9:1mfalme wa Dori katika kilima cha Dori, mmoja; na mfalme wa makabila katika Gilgali, mmoja; 24na mfalme wa Tirsa, mmoja; wafalme hao wote walikuwa ni thelathini na mmoja.