Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yos UTANGULIZI

UTANGULIZI
Kitabu hiki cha Yoshua kimepewa jina la mtu aliyerithi uongozi kutoka kwa Musa (Hesabu 27:18-23). Yoshua ni wa kabila la Efraimu. Waisraeli walipotoka Misri alikuwa bado kijana. Safarini jangwani Musa alimteua kuwa kiongozi (Kut 17:8-16; 33:11; Hes 13:8, 16). Yamkinika Yoshua alianza kuwaongoza Waisraeli akiwa na umri wa miaka kati ya 70 na 80. Alikufa akiwa na umri wa miaka 110, akazikwa Timnath-sera kwenye milima ya Efraimu (24:29-30). Yoshua anahesabiwa kuwa kiongozi hodari, shujaa na mcha Mungu. Aliamini kuwa mafanikio yao hayatokani na kutegema nguvu na uhodari wa jeshi lao bali utii mkamilifu kwa Agano lao na Mungu.
Kitabu cha Yoshua kinaendeleza masimulizi ya kitabu cha Hesabu kwa kuanzia kile cha Hesabu kilipoishia. Aidha kina mkazo maalumu juu ya historia ya wokovu. Mungu alichagua taifa la Israeli; pia ana wivu kwa taifa lake, anataka limtumikie yeye tu (21:43-45; 23:11; 24:14).
Kinasimulia juu ya Waisraeli kuvuka Yordani, kushambulia, kushinda na kuteka nchi ya Kanaani, kugawanya nchi hiyo katika makabila ya Waisraeli na kuweka miji maalumu kwa wakimbizi vinatokana na uaminifu na utendaji wa Mungu. Kabla ya kufa kwake, Yoshua anakumbusha kuwa hawana budi kumtii Mungu na Agano lake.
Yaliyomo:
1. Waisraeli waiteka Kanaani, Sura 1-12
2. Kugawana nchi ya Kanaani, Sura 13-21
3. Kurudi kwa makabila ya mashariki, Sura 22
4. Hotuba ya mwisho ya Yoshua, Sura 23
5. Agano la kumtumikia Mungu, Sura 24:1-28
6. Vifo na mazishi ya Yoshua na Eleazari, Sura 24:29-33

Iliyochaguliwa sasa

Yos UTANGULIZI: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia