Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mt 24

24
Kuharibiwa kwa Hekalu Kwatabiriwa
1 # Mk 13:1-37; Lk 21:5-36 Yesu akaenda zake, akatoka hekaluni; wanafunzi wake wakamwendea ili kumwonyesha majengo ya hekalu. 2#Lk 19:44Naye akajibu akawaambia, Hamyaoni haya yote? Amin, nawaambieni, Halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa.
Ishara za Mwisho wa Nyakati
3Hata alipokuwa ameketi katika mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamwendea kwa faragha, wakisema, Tuambie, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya kuja kwako, na ya mwisho wa dunia? 4Yesu akajibu, akawaambia, Angalieni, mtu asiwadanganye. 5#Mt 24:24; Yn 5:43; Mdo 5:36,37; 1 Yoh 2:18Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ni Kristo; nao watadanganya wengi. 6#Dan 2:28Nanyi mtasikia habari za vita na matetesi ya vita; angalieni, msitishwe; maana hayo hayana budi kutukia; lakini ule mwisho bado. 7#Isa 19:2; 2 Nya 15:6Kwa maana taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwa na njaa, na matetemeko ya nchi mahali mahali. 8Hayo yote ndiyo mwanzo wa utungu.
Mateso Yatabiriwa
9 # Mt 10:17,22; Yn 16:2 Wakati huo watawasaliti ninyi mpate dhiki, nao watawaua; nanyi mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa yote kwa ajili ya jina langu. 10#Dan 11:41Ndipo wengi watakapojikwaa, nao watasalitiana, na kuchukiana. 11#Mt 7:15; 1 Yoh 4:1Na manabii wengi wa uongo watatokea, na kudanganya wengi. 12#2 The 2:10; 2 Tim 3:1-5Na kwa sababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa. 13#Mt 10:22; Ufu 13:10Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka. 14#Mt 28:19; 10:18Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.
Chukizo la Uharibifu
15 # Dan 9:27; 11:31; 12:11 Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli, limesimama katika patakatifu (asomaye na afahamu), 16ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani; 17#Lk 17:31naye aliye juu ya dari asishuke kuvichukua vitu vilivyomo nyumbani mwake; 18wala aliye shambani asirudi nyuma kuichukua nguo yake. 19Ole wao wenye mimba na wanyonyeshao siku hizo! 20#Mdo 1:12Ombeni, ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi, wala siku ya sabato. 21#Dan 12:1; Ufu 7:14; Yoe 2:2Kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe. 22Na kama siku hizo zisingalifupizwa, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule zitafupizwa siku hizo. 23Wakati huo mtu akiwaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko kule msisadiki. 24#Mt 5:11; Kum 13:1-3; 2 The 2:8,9Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule. 25Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele. 26#Lk 17:23-24Basi wakiwaambia, Yuko jangwani, msitoke; yumo nyumbani, msisadiki. 27Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. 28#Ayu 39:30; Hab 1:8; Lk 17:37Kwa kuwa po pote ulipo mzoga, ndipo watakapokusanyika tai.
Kuja kwa Mwana wa Adamu
29 # Isa 13:10; 34:4; Eze 32:7; Yoe 2:10; 3:4,15; Ufu 6:12-13; 2 Pet 3:10 Lakini mara, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika; 30#Dan 7:13; Zek 12:10-14; Ufu 1:7; 19:11; Mt 26:64ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi. 31#1 Kor 15:52; 1 The 4:16; Ufu 8:1,2; Isa 27:13; Zek 2:6; Kum 30:4Naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu.
Funzo kutoka kwa Mtini
32Basi kwa mtini jifunzeni mfano; tawi lake likiisha kuchipuka na kuchanua majani, mwatambua ya kuwa wakati wa mavuno u karibu; 33nanyi kadhalika, myaonapo hayo yote, tambueni ya kuwa yu karibu, milangoni. 34Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia. 35#Mt 5:18Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
Haja ya kuwa Waangalifu
36 # 1 The 5:1,2 Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake. 37#Mwa 6:5-8; Lk 17:26,27Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. 38#2 Pet 3:5,6; Mwa 7:7Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina, 39#Mwa 7:6-24wasitambue, hata Gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. 40#Lk 17:35,36Wakati ule watu wawili watakuwako kondeni; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa; 41wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa.
42 # Mt 25:13 Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu. 43#Lk 12:39-40Lakini fahamuni neno hili; kama mwenye nyumba angaliijua ile zamu mwivi atakayokuja, angalikesha, wala asingaliiacha nyumba yake kuvunjwa. 44#Ufu 16:15Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja.
Mtumwa Mwaminifu au asiye Mwaminifu
45Ni nani basi yule mtumwa mwaminifu mwenye akili, ambaye bwana wake alimweka juu ya nyumba yake, awape watu chakula kwa wakati wake? 46Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta akifanya hivyo. 47#Mt 25:21,23Amin, nawaambieni, atamweka juu ya vitu vyake vyote. 48#Mhu 8:11Lakini mtumwa yule mbaya akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia; 49akaanza kuwapiga wajoli wake, na kula na kunywa pamoja na walevi; 50bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani, na saa asiyojua, 51#Mt 8:12atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wanafiki; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.

Iliyochaguliwa sasa

Mt 24: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia