Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hes 26

26
Sensa ya Kizazi Kipya
1 # Hes 1:1-46 Ikawa baada ya hilo pigo, BWANA akanena na Musa na Eleazari, mwana wa Haruni kuhani, na kuwaambia, 2#Kut 30:12; 38:25; Hes 1:2Fanya jumla ya mkutano wote wa wana wa Israeli, tangu umri wa miaka ishirini, na zaidi, kwa nyumba za baba zao, hao wote katika Israeli wawezao kutoka kuenenda vitani. 3#Kum 4:46-49; 34:1Kisha Musa na Eleazari kuhani wakanena nao katika nchi tambarare za Moabu karibu na mto wa Yordani, huko Yeriko, wakawaambia, 4Fanyeni jumla ya watu, tangu umri wa miaka ishirini, na zaidi; kama BWANA alivyomwagiza Musa na wana wa Israeli, hao waliotoka nchi ya Misri.
5 # Mwa 29:32; 46:8; 1 Nya 5:1; Ufu 7:5 Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Israeli, wana wa Reubeni; wa Hanoki, jamaa ya Wahanoki; na wa Palu, jamaa ya Wapalu; 6na wa Hesroni, jamaa ya Wahesroni; na wa Karmi, jamaa ya Wakarmi. 7Hizi ndizo jamaa za Wareubeni; na hao waliohesabiwa kwao walikuwa arobaini na tatu elfu na mia saba na thelathini. 8Na wana wa Palu; Eliabu. 9#Hes 16:1,2; 27:3; Kum 11:6; Isa 65:16; Zab 106:17; Yud 1:11Na wana wa Eliabu; Nemueli, na Dathani, na Abiramu. Hawa ndio Dathani na Abiramu waliochaguliwa na mkutano, ambao walishindana na Musa na Haruni katika mkutano wa Kora, hapo waliposhindana na BWANA; 10#Hes 16:38; 1 Sam 2:34; Ayu 31:3; Zab 145:20; Yer 29:22; 1 Kor 10:6; 2 Pet 2:6; Yud 1:7nchi ikafunua kinywa chake, na kuwameza pamoja na Kora, mkutano huo ulipokufa; wakati moto ulipowateketeza watu mia mbili na hamsini, nao wakawa ishara. 11#Kut 6:24; 1 Nya 6:22; Eze 18:20Pamoja na hayo, hao wana wa Kora hawakufa.
12 # Mwa 46:10; Kut 6:15; 1 Nya 4:24 Na wana wa Simeoni kwa jamaa zao; wa Yemueli, jamaa ya Wayemueli; wa Yamini, jamaa ya Wayamini; na Yakini, jamaa ya Wayakini; 13#Mwa 46:10wa Sohari, jamaa ya Wasohari; wa Shauli, jamaa ya Washauli. 14Hizi ndizo jamaa za Wasimeoni, watu ishirini na mbili elfu na mia mbili.
15Na wana wa Gadi kwa jamaa zao; wa Sifoni, jamaa ya Wasifoni; wa Hagi, jamaa ya Wahagi; wa Shuni, jamaa ya Washuni; 16wa Ezboni, jamaa ya Waezboni; wa Eri, jamaa ya Waeri; 17#Mwa 46:16wa Arodi, jamaa ya Waarodi; wa Areli, jamaa ya Waareli. 18Hizi ndizo jamaa za wana wa Gadi kama waliohesabiwa kwao, arobaini elfu na mia tano.
19 # Mwa 38:2; 46:12; 1 Nya 2:3 Na wana wa Yuda, Eri na Onani; na hao Eri na Onani wakafa katika nchi ya Kanaani. 20#Mwa 49:8; Ufu 7:5Na wana wa Yuda kwa jamaa zao; wa Shela, jamaa ya Washela; wa Peresi, jamaa ya Waperesi; wa Zera, jamaa ya Wazera. 21Na wana wa Peresi walikuwa; wa Hesroni, jamaa ya Wahesroni; wa Hamuli, jamaa ya Wahamuli. 22Hizi ndizo jamaa za Yuda kama waliohesabiwa kwao, sabini na sita elfu na mia tano.
23 # Mwa 46:13; 49:14 Na wana wa Isakari kwa jamaa zao; wa Tola, jamaa ya Watola; wa Puva, jamaa ya Wapuva; 24wa Yashubu, jamaa ya Wayashubu; wa Shimroni, jamaa ya Washimroni. 25Hizi ndizo jamaa za Isakari kama waliohesabiwa kwao, sitini na nne elfu na mia tatu.
26 # Mwa 46:14; 49:13 Na wana wa Zabuloni kwa jamaa zao; wa Seredi, jamaa ya Waseredi; wa Eloni, jamaa ya Waeloni; wa Yaleeli, jamaa ya Wayaleeli. 27Hizi ndizo jamaa za Wazabuloni kama waliohesabiwa kwao, sitini elfu na mia tano.
28 # Mwa 41:51; 46:20; 48:3,13-20 Na wana wa Yusufu kwa jamaa zao; Manase na Efraimu. 29#Hes 32:39; 36:1Wana wa Manase; wa Makiri, jamaa ya Wamakiri; na Makiri akamzaa Gileadi; wa Gileadi, jamaa ya Wagileadi. 30#Yos 17:2Hawa ndio wana wa Gileadi; wa Abiezeri, jamaa ya Waabiezeri; wa Heleki, jamaa ya Waheleki; 31na wa Asrieli, jamaa ya Waasrieli; na wa Shekemu, jamaa ya Washekemu; 32na wa Shemida, jamaa ya Washemida; na wa Heferi, jamaa ya Waheferi. 33#Hes 27:1; 36:11; Yos 17:3Na Selofehadi mwana wa Heferi hakuwa na wana waume, isipokuwa wa kike; na majina ya hao binti za Selofehadi ni haya, Mala, na Noa, na Hogla, na Milka, na Tirsa. 34Hizi ndizo jamaa za Manase; na waliohesabiwa kwao walikuwa ni hamsini na mbili elfu na mia saba.
35 # 1 Nya 7:20 Na wana wa Efraimu kwa jamaa zao; wa Shuthela, jamaa ya Washuthela; wa Beredi, jamaa ya Waberedi; wa Tahathi, jamaa ya Watahathi. 36Na wana wa Shuthela ni hawa; wa Erani, jamaa ya Waerani. 37#Kum 33:13-17Hizi ndizo jamaa za wana wa Efraimu kama waliohesabiwa kwao, thelathini na mbili elfu na mia tano. Hao ndio wana wa Yusufu kwa jamaa zao.
38 # Mwa 46:21; 1 Nya 7:6; 8:1 Na wana wa Benyamini kwa jamaa zao; wa Bela, jamaa ya Wabela; na wa Ashbeli, jamaa ya Waashbeli; wa Ahiramu, jamaa ya Waahiramu; 39#Mwa 46:21; 1 Nya 7:12wa Shufamu, jamaa ya Washufamu; wa Hufamu, jamaa ya Wahufamu. 40#1 Nya 8:3Na wana wa Bela walikuwa Ardi na Naamani; wa Ardi, jamaa ya Waardi; wa Naamani, jamaa ya Wanaamani. 41Hao ndio wana wa Benyamini kwa jamaa zao; na waliohesabiwa kwao walikuwa arobaini na tano elfu na mia sita.
42 # Mwa 46:23; 49:16; Hes 1:38,39; Kum 33:22 Na wana wa Dani ni hawa kwa jamaa zao; wa Shuhamu, jamaa ya Washuhamu. Hizi ndizo jamaa za Dani kwa jamaa zao. 43Jamaa zote za Washuhamu, kama waliohesabiwa kwao, walikuwa sitini na nne elfu na mia nne.
44 # Mwa 46:17; 1 Nya 7:30 Na wana wa Asheri kwa jamaa zao; wa Imna, jamaa ya Waimna; wa Ishvi jamaa ya Waishvi; wa Beria, jamaa ya Waberia. 45Wa wana wa Beria; wa Heberi, jamaa ya Waheberi; wa Malkieli, jamaa ya Wamalkieli. 46Na jina la binti wa Asheri aliitwa Sera. 47Hizi ndizo jamaa za wana wa Asheri kama waliohesabiwa kwao, hamsini na tatu elfu na mia nne.
48 # Mwa 46:24; 1 Nya 7:13 Na wana wa Naftali kwa jamaa zake; wa Yaseeli, jamaa ya Wayaseeli; na wa Guni, jamaa ya Waguni; 49#1 Nya 7:13wa Yeseri, jamaa ya Wayeseri, wa Shilemu jamaa ya Washilemu. 50Hizi ndizo jamaa za Naftali kwa jamaa zao; na waliohesabiwa kwao walikuwa arobaini na tano elfu na mia nne.
51 # 1:46; 2:32 Hao ndio waliohesabiwa katika wana wa Israeli, mia sita na moja elfu, na mia saba na thelathini (601,730).
52 # Hes 34:13; Yos 14:1-2 Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 53Watu hawa watagawanyiwa nchi hiyo iwe urithi wao, vile vile kama hesabu ya majina yao ilivyo. 54#Hes 33:54Hao waliozidi hesabu yao utawapa urithi zaidi, na hao waliopunguka hesabu yao, utawapa urithi kama upungufu wao; kila mtu kama watu wake walivyohesabiwa, ndivyo atakavyopewa urithi wake. 55#Hes 34:13; Yos 11:23; 14:2Lakini nchi itagawanywa kwa kura; kwa majina ya kabila za baba zao, ndivyo watakavyopata urithi. 56Kama kura itakavyokuwa, ndivyo urithi wao utakavyogawanywa kati yao, hao wengi na hao wachache.
57 # Mwa 46:11; Kut 6:16; 1 Nya 6:1,16 Na hao waliohesabiwa katika Walawi kwa jamaa zao ni hawa; wa Gershoni, jamaa ya Wagershoni; na wa Kohathi, jamaa ya Wakohathi; na wa Merari, jamaa ya Wamerari. 58Hizi ndizo jamaa za Lawi; jamaa ya Walibni, na jamaa ya Wahebroni, na jamaa ya Wamala, na jamaa ya Wamushi jamaa ya Wakora. Na Kohathi alimzaa Amramu. 59Na jina la mke wa Amramu aliitwa Yokebedi, binti wa Lawi, ambaye alizaliwa kwake Lawi huko Misri; na huyo Yokebedi akamzalia Amramu Haruni, na Musa, na Miriamu umbu lao. 60#Hes 3:2Tena kwake Haruni walizaliwa hawa, Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari. 61#Law 10:1-2; Hes 3:4; 1 Nya 24:2Tena Nadabu na Abihu wakafa, hapo waliposongeza moto wa kigeni mbele za BWANA. 62#Hes 3:39; 1:49; 18:20-24; 35:2-8; Kum 10:9; 14:27-29; Yos 13:14; 14:3Na hao waliohesabiwa kwao walikuwa ishirini na tatu elfu, kila mwanamume tangu huyo aliyepata umri wa mwezi mmoja, na zaidi; kwa kuwa hawakuhesabiwa katika wana wa Israeli, kwa sababu hawakupewa urithi katika wana wa Israeli.
63Hao ndio waliohesabiwa na Musa na Eleazari kuhani; ambao waliwahesabu wana wa Israeli katika nchi tambarare za Moabu, karibu na Yordani, hapo Yeriko. 64#Hes 1:1; Kum 2:14,15Lakini katika watu hao hapakuwa na mtu hata mmoja wa wale waliohesabiwa na Musa na Haruni kuhani; waliowahesabu wana wa Israeli katika bara ya Sinai. 65#Hes 14:26-35; Kum 32:49,50; Zab 90:3-8; Rum 11:22; 1 Kor 10:5; Ebr 3:17,18; Yud 1:5; Hes 14:30; 32:12; Kum 1:36,38; Yos 14:10Kwa kuwa BWANA alisema juu yao, Hapana budi watakufa nyikani. Napo hapakusalia mtu mmoja miongoni mwao, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune, na Yoshua mwana wa Nuni.

Iliyochaguliwa sasa

Hes 26: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia