10
KITABU CHA PILI
Mithali za Sulemani.
1Mwana mwenye hekima humfurahisha babaye;
Bali mwana mpumbavu ni mzigo wa mamaye.
2 #
Zab 49:6; Lk 12:19; Dan 4:27 Hazina za uovu hazifaidii kitu;
Bali haki huokoa na mauti.
3 #
Zab 10:14
BWANA hataiacha nafsi ya mwenye haki ife na njaa;
Bali tamaa ya mtu mwovu huisukumia mbali.
4 #
Mit 13:4
Atendaye mambo kwa mkono mlegevu huwa maskini;
Bali mkono wake aliye na bidii hutajirisha.
5Akusanyaye wakati wa hari ni mwana mwenye hekima;
Bali asinziaye wakati wa mavuno ni mwana mwenye kuaibisha.
6 #
Est 7:8
Baraka humkalia mwenye haki kichwani;
Bali jeuri hufunika kinywa chake mtu mwovu.
7 #
Zab 9:5,6; Mhu 8:10 Kuwakumbuka wenye haki huwa na baraka;
Bali jina la mtu mwovu litaoza.
8Aliye na akili moyoni mwake atapokea agizo;
Bali mpumbavu mwenye maneno mengi ataanguka.
9 #
Zab 23:4; Isa 33:15,16 Aendaye kwa unyofu huenda salama;
Bali apotoshaye njia zake atajulikana.
10Akonyezaye kwa jicho huleta masikitiko;
Bali mpumbavu mwenye maneno mengi ataanguka.
11 #
Zab 37:30; 107:42 Kinywa chake mwenye haki ni chemchemi ya uzima;
Bali jeuri hufunika kinywa chake mtu mwovu,
12 #
Yak 5:20; 1 Pet 4:8; 1 Kor 13:4 Kuchukiana huondokesha fitina;
Bali kupendana husitiri makosa yote.
13 #
Lk 4:22
Hekima hupatikana midomoni mwa mwenye ufahamu;
Bali fimbo hufaa kwa mgongo wake asiye na ufahamu.
14Watu wenye akili huweka akiba ya maarifa;
Bali kinywa cha mpumbavu ni uangamivu ulio karibu.
15 #
Ayu 31:24; Mit 18:11; Lk 12:19; 1 Tim 6:17 Mali ya mtu tajiri ni mji wake wa nguvu;
Uangamivu wa maskini ni umaskini wao.
16Kazi yake mwenye haki huuelekea uzima;
Mazao ya wabaya huuelekea dhambi.
17Akubaliye kurudiwa huwa katika njia ya uzima;
Bali yeye aachaye maonyo hukosa.
18Yeye afichaye chuki ana midomo ya uongo,
Na yeye asingiziaye ni mpumbavu.
19 #
Mhu 5:3; Zab 39:1; Mit 17:27,28; Yak 1:19 Katika wingi wa maneno hapakosi kuwa na maovu;
Bali yeye azuiaye midomo yake hufanya akili.
20Ulimi wa mwenye haki ni kama fedha teule;
Moyo wa mtu mbaya haufai kitu.
21Midomo ya mwenye haki hulisha watu wengi;
Bali wapumbavu hufa kwa kuwa hawana ufahamu.
22 #
Mwa 12:2; Kum 8:17,18; 1 Sam 2:7,8; 1 Tim 4:8 Baraka ya BWANA hutajirisha,
Wala hachanganyi huzuni nayo.
23Kwa mpumbavu kutenda maovu ni kama mchezo;
Bali mtu mwenye ufahamu ana hekima.
24 #
Ayu 15:21; Mt 5:6 Aogopacho mtu asiye haki ndicho kitakachomjilia;
Na wenye haki watapewa matakwa yao.
25 #
Zab 15:5; Mt 7:24; 1 Tim 6:19 Kisulisuli kikiisha pita asiye haki hayuko tena;
Bali mwenye haki ni msingi wa milele.
26Kama siki menoni, na kama moshi machoni,
Ndivyo alivyo mtu mvivu kwao wamtumao.
27 #
Mhu 7:17
Kumcha BWANA kwaongeza siku za mtu;
Bali miaka yao wasio haki itapunguzwa.
28 #
Zab 16:9; Rum 5:2; Ayu 8:13 Matumaini yao wenye haki yatakuwa furaha;
Bali kutaraji kwao wasio haki kutapotea.
29 #
Zek 10:12; Flp 4:13; Isa 40:31; Zab 1:6 Njia ya BWANA ni kimbilio lake mtu mkamilifu;
Bali ni uharibifu kwao watendao maovu.
30Mwenye haki hataondolewa milele;
Bali wasio haki hawatakaa katika nchi.
31Kinywa cha mwenye haki hutoa hekima;
Bali ulimi wa ukaidi utakatiliwa mbali.
32Midomo ya mwenye haki huyajua yatakayokubaliwa;
Bali kinywa chao wasio haki hunena ukaidi.