22
1Heri kuchagua jina jema kuliko mali nyingi;
Na neema kuliko fedha na dhahabu.
2 #
Zab 49:1,2 Tajiri na maskini hukutana pamoja;
BWANA ndiye aliyewaumba wote wawili.
3 #
Isa 26:20
Mwenye busara huyaona mabaya na kujificha;
Bali wajinga huendelea mbele wakaumia.
4Thawabu ya unyenyekevu ambao ni kumcha BWANA
Ni utajiri, na heshima, nayo ni uzima.
5 #
1 Yoh 5:18
Miiba na mitego huwa katika njia ya mshupavu;
Yeye aitunzaye nafsi yake atakuwa mbali nayo.
6Mlee mtoto katika njia impasayo,
Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.
7Tajiri humtawala maskini,
Naye akopaye ni mtumwa wake akopeshaye.
8 #
Ayu 4:8; Hos 10:13 Yeye apandaye uovu atavuna msiba,
Na fimbo ya ghadhabu yake itakoma.
9Mwenye jicho la ukarimu atabarikiwa;
Maana huwapa maskini chakula chake.
10Mtupe nje mwenye dharau, na ugomvi utatoka;
Naam, fitina na fedheha zitakoma.
11Apendaye usafi wa moyo, na neema ya midomo;
Mfalme atakuwa rafiki yake.
12Macho ya BWANA humhifadhi mwenye maarifa;
Bali huyapindua maneno ya mtu haini.
13Mtu mvivu husema, Simba yuko nje;
Nitauawa katika njia kuu.
14 #
Mit 2:16; Mhu 7:26 Kinywa cha malaya ni shimo refu;
Anayechukiwa na BWANA atatumbukia ndani yake.
15Ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto;
Lakini fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali.
16 #
Ayu 20:19-23; 34:26-28; Zab 12:5; Mhu 5:8; Amo 2:6-8; 5:11; Isa 3:14,15; Yak 2:13 Yeye awaoneaye maskini ili kuongeza mapato,
Naye ampaye tajiri, hupata hasara.
KITABU CHA TATU
Maneno ya Wenye Hekima
17Tega sikio lako uyasikie maneno ya wenye hekima, na kuuelekeza moyo wako kwa maarifa yangu; 18maana ni vizuri kuyahifadhi ndani yako, hali yakithibitika pamoja midomoni mwako. 19Ili matumaini yako uyaweke kwa BWANA, leo nimekujulisha wewe haya, naam, wewe. 20Je! Sikukuandikia mambo makuu juu ya mashauri na juu ya maarifa; 21#1 Pet 3:15ili kukujulisha hakika ya maneno ya kweli, uwarudishie wakutumao maneno ya kweli?
22 #
Mal 3:5
Usimnyang’anye maskini, kwa kuwa ni maskini;
Wala usimdhulumu mtu mnyonge langoni;
23Kwa sababu BWANA atawatetea;
Naye atawateka uhai wao waliowateka.
24Usifanye urafiki na mtu mwenye hasira nyingi;
Wala usiende na mtu wa ghadhabu nyingi;
25Usije ukajifunza njia zake;
Na kujipatia nafsi yako mtego.
26Usiwe mmoja wao wawekao rehani;
Au walio wadhamini kwa deni za watu;
27Kama huna kitu cha kulipa;
Kwani ukaondolee kitanda chako chini yako?
28Usiiondoe alama ya mpaka wa zamani,
Uliowekwa na baba zako.
29 #
1 Fal 11:28; Mit 10:4; Mhu 9:10; Mt 25:21; Rum 12:11 Je! Wamwona mtu mwenye bidii katika kazi zake?
Huyo atasimama mbele ya wafalme;
Hatasimama mbele ya watu wasio na cheo.