Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mit 27

27
1 # Yak 4:13-16; Lk 12:19 Usijisifu kwa ajili ya kesho;
Kwa maana hujui yatakayozaliwa na siku moja.
2Mwingine na akusifu wala si kinywa chako mwenyewe;
Mtu mgeni wala si midomo yako wewe.
3 # Est 1:12 Jiwe ni zito, na mchanga hulemea;
Lakini ghadhabu ya mpumbavu ni nzito kuliko hivi vyote viwili.
4 # 1 Yoh 3:12 Ghadhabu ni kali, na hasira ni gharika;
Lakini ni nani awezaye kusimama mbele ya wivu.
5 # Gal 2:14 Lawama ya wazi ni heri,
Kuliko upendo uliositirika.
6Jeraha utiwazo na rafiki ni amini;
Bali kubusu kwa adui ni kwingi sana.
7Nafsi iliyoshiba hukinai sega la asali;
Bali nafsi yenye njaa huona kila kitu kichungu kuwa kitamu.
8 # Ayu 39:14 Kama ndege aendaye huko na huko mbali na kitundu chake;
Ndivyo alivyo mtu aendaye huko na huko mbali na mahali pake.
9Marhamu na manukato huufurahisha moyo;
Kadhalika utamu wa rafiki ya mtu utokao katika kusudi la moyo wake.
10Usimwache rafiki yako mwenyewe, wala rafiki ya baba yako,
Wala usiende nyumbani mwa ndugu yako siku ya msiba wako.
Afadhali jirani aliye karibu kuliko ndugu aliye mbali.
11 # Zab 119:42 Mwanangu, uwe na hekima na kunifurahisha moyo wangu;
Ili nipate kumjibu anilaumuye.
12 # Isa 32:2 Mwenye busara huyaona mabaya na kujificha;
Bali wajinga huendelea mbele wakaumia.
13Twaa nguo yake amdhaminiye mgeni;
Mtoza rehani aliye mdhamini wa malaya.
14 # Zab 12:2 Mtu ambarikiye mwenzake kwa sauti kuu asubuhi na mapema;
Itahesabiwa kuwa ni laana kwake.
15Kutona-tona daima siku ya mvua nyingi,
Na mwanamke mgomvi ni sawasawa;
16Atakaye kumzuia huyo huuzuia upepo;
Na mkono wake wa kuume hukuta mafuta.
17Chuma hunoa chuma;
Ndivyo mtu aunoavyo uso wa rafiki yake.
18 # Kum 20:6; 1 Fal 11:8; Mit 12:24; 1 Kor 3:8 Yeye autunzaye mtini atakula matunda yake;
Naye amhudumiaye bwana wake ataheshimiwa.
19Kama uso ufananavyo na uso katika maji;
Kadhalika moyo wa mtu na mwenzake.
20 # Mit 30:15,16; Hab 2:5 Kuzimu na Uharibifu havishibi;
Wala macho ya wanadamu hayashibi.
21Kalibu ni kwa fedha, na tanuru kwa dhahabu;
Na mtu hujaribiwa kwa sifa zake.
22Hata ukimtwanga mpumbavu kwa mchi kinuni pamoja na ngano;
Upumbavu wake hautamtoka.
23Fanya bidii kuijua hali ya makundi yako;
Na kuwaangalia sana ng’ombe zako.
24Kwa maana mali haziwi za milele;
Na taji je! Yadumu tangu kizazi hata kizazi?
25Manyasi huchukuliwa, na majani mabichi huonekana,
Na maboga ya milimani hukusanyika.
26Wana-kondoo hufaa kwa mavazi yako;
Na mbuzi ni thamani ya shamba
27Tena yatakuwapo maziwa ya mbuzi,
Ya kukutosha kwa chakula chako,
Na chakula cha watu wa nyumbani mwako,
Na posho la vijakazi vyako.

Iliyochaguliwa sasa

Mit 27: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia