Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 104

104
Mungu Muumba na Atoaye
1Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA.
Wewe, BWANA, Mungu wangu,
Umejifanya mkuu sana;
Umejivika heshima na adhama.
2Umejivika nuru kama vazi;
Umezitandika mbingu kama pazia;
3 # Amo 9:6; Isa 19:1 Na kuziweka nguzo za orofa zake majini.
Huyafanya mawingu kuwa gari lake,
Na kwenda juu ya mabawa ya upepo,
4 # Ebr 1:7 Huwafanya malaika zake kuwa pepo,
Na watumishi wake kuwa moto wa miali.
5Uliiweka nchi juu ya misingi yake,
Isitikisike milele.
6Uliifunika kwa vilindi kama kwa vazi,
Maji yalikuwa yakisimama juu ya milima.
7Kwa kukemea kwako yakakimbia,
Kwa sauti ya radi yako yakaenda zake kasi,
8 # Ayu 38:10 Yakapanda milima, yakatelemka mabondeni,
Mpaka mahali ulipoyatengenezea.
9 # Ayu 26:10; Zab 33:7; Yer 5:22; Mwa 9:11 Umeweka mpaka yasiupite,
Wala yasirudi kuifunikiza nchi.
10Hupeleka chemchemi katika mabonde;
Zapita kati ya milima;
11Zamnywesha kila mnyama wa kondeni;
Punda mwitu huzima kiu yao.
12Kandokando hukaa ndege wa angani;
Kati ya matawi hutoa sauti zao.
13Huinywesha milima toka orofa zake;
Nchi imeshiba mazao ya kazi zako.
14 # Mwa 1:29,30; Zab 147:8; 136:25; Ayu 28:5 Huyameesha majani kwa makundi,
Na maboga kwa matumizi ya mwanadamu;
Ili atoe chakula katika nchi,
15 # Amu 9:13; Mit 31:6,7; Mhu 10:19; Yer 31:12; Yn 2:9,10 Na divai imfurahishe mtu moyo wake.
Aung’aze uso wake kwa mafuta,
Na mkate umburudishe mtu moyo wake.
16 # Hes 24:6; Zab 29:5 Miti ya BWANA nayo imeshiba,
Mierezi ya Lebanoni aliyoipanda.
17Ndimo ndege wafanyamo vitundu vyao,
Na korongo, misunobari ni nyumba yake.
18 # Mit 30:26 Milima mirefu ndiko waliko mbuzi wa mwitu,
Na magenge ni kimbilio la wibari.
19 # Mwa 1:14; Ayu 38:12 Aliufanya mwezi kwa ajili ya nyakati,
Jua latambua kuchwa kwake.
20 # Isa 45:7 Wewe hufanya giza, kukawa usiku,
Ndipo atambaapo kila mnyama wa mwitu.
21 # Ayu 38:39 Wana-simba hunguruma wakitaka mawindo,
Ili kutafuta chakula chao kwa Mungu.
22Jua lachomoza, wanakwenda zao,
Na kujilaza mapangoni mwao.
23 # Mwa 3:19 Mwanadamu atoka kwenda zake kazini,
Na kwenye utumishi wake mpaka jioni.
24 # Mwa 1:20-22 Ee BWANA, jinsi yalivyo mengi matendo yako!
Kwa hekima umevifanya vyote pia.
Dunia imejaa mali zako.
25Bahari iko kule, kubwa na upana,
Ndimo mlimo viendavyo visivyohesabika,
Viumbe hai vidogo kwa vikubwa.
26 # Ayu 41:1; Zab 74:14; Isa 27:1 Ndimo zipitamo merikebu,
Ndimo alimo lewiathani uliyemwumba acheze humo.
27 # Rum 11:36 Hao wote wanakungoja Wewe,
Uwape chakula chao kwa wakati wake.
28Wewe huwapa,
Wao wanakiokota;
Wewe waukunjua mkono wako,
Wao wanashiba mema;
29 # Mhu 12:7 Wewe wauficha uso wako,
Wao wanafadhaika;
Waiondoa pumzi yao, wanakufa,
Na kuyarudia mavumbi yao,
30 # Isa 32:15 Waipeleka roho yako, wanaumbwa,
Nawe waufanya upya uso wa nchi.
31Utukufu wa BWANA na udumu milele;
BWANA na ayafurahie matendo yake.
32 # Hab 3:10 Aitazama nchi, inatetemeka;
Aigusa milima, inatoka moshi.
33Nitamwimbia BWANA maadamu ninaishi;
Nitamshangilia Mungu wangu nikiwa hai;
34Kutafakari kwangu na kuwe kutamu kwake;
Mimi nitamfurahia BWANA.
35 # Mit 2:22 Wenye dhambi waangamizwe katika nchi,
Watendao ubaya wasiwepo tena.
Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA.

Iliyochaguliwa sasa

Zab 104: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia