Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 13

13
Sala ya Ukombozi kutoka kwa Adui
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.
1 # Kum 31:17; Ayu 13:24; Zab 22:1; Isa 59:2 Ee BWANA, hata lini utanisahau, hata milele?
Hata lini utanificha uso wako?
2Hata lini nifanye mashauri nafsini mwangu,
Nikihuzunika moyoni mchana kutwa?
Hata lini adui yangu atukuke juu yangu?
3 # Ezr 9:8; Zab 18:28; Lk 2:32; Ufu 21:23; Zab 76:5,6; Isa 37:36; Yer 51:39; Efe 5:14 Ee BWANA, Mungu wangu, uangalie, uniitikie;
Uyatie nuru macho yangu,
Nisije nikalala usingizi wa mauti.
4Adui yangu asije akasema, Nimemshinda;
Watesi wangu wasifurahi ninapoondoshwa.
5 # 2 Nya 20:12 Nami nimezitumainia fadhili zako;
Moyo wangu na uufurahie wokovu wako.
6Naam, nimwimbie BWANA,
Kwa kuwa amenitendea kwa ukarimu.

Iliyochaguliwa sasa

Zab 13: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia