Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 15

15
Nani Atakaa katika Patakatifu pa Mungu?
Zaburi ya Daudi.
1 # Zab 2:5 BWANA, ni nani atakayekaa
Katika hema yako?
Ni nani atakayefanya maskani yake
Katika kilima chako kitakatifu?
2 # Zab 84:11; Isa 33:15,16 Ni mtu aendaye kwa ukamilifu,
Na kutenda haki.
Asemaye kweli kwa moyo wake,
3Asiyesingizia kwa ulimi wake.
Wala hakumtenda mwenziwe mabaya,
Wala hakumsengenya jirani yake.
4 # Yos 9:18-20 Machoni pake mtu asiyefaa hudharauliwa,
Bali huwaheshimu wamchao BWANA
Ingawa ameapa kwa hasara yake,
Hayabadili maneno yake.
5 # Eze 18:8,9 Hakutoa fedha yake apate kula riba,
Hakutwaa rushwa amwangamize asiye na hatia.
Mtu atendaye mambo hayo
Hataondoshwa milele.

Iliyochaguliwa sasa

Zab 15: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia