Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 2:1-6

Zab 2:1-6 SUV

Mbona mataifa wanafanya ghasia, Na makabila wanatafakari ubatili? Wafalme wa dunia wanajipanga, Na wakuu wanafanya shauri pamoja, Juu ya BWANA, Na juu ya masihi wake, Na tuvipasue vifungo vyao, Na kuzitupia mbali nasi kamba zao. Yeye aketiye mbinguni anacheka, Bwana anawafanyia dhihaka. Ndipo atakaposema nao kwa hasira yake, Na kuwafadhaisha kwa ghadhabu yake. Nami nimemweka mfalme wangu Juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu.