Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 23

23
Mchungaji Mwema
Zaburi ya Daudi.
1 # Yn 10:11; 1 Pet 2:25 BWANA ndiye mchungaji wangu,
Sitapungukiwa na kitu.
2 # Ufu 7:17; Eze 34:14 Katika malisho ya majani mabichi hunilaza,
Kando ya maji ya utulivu huniongoza.
3Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza
Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.
4 # Zab 46:11; Isa 8:10; Zek 8:23; Mt 1:23; Mdo 18:9,10 Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti,
Sitaogopa mabaya;
Kwa maana Wewe upo pamoja nami,
Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.
5Waandaa meza mbele yangu,
Machoni pa watesi wangu.
Umenipaka mafuta kichwani pangu,
Na kikombe changu kinafurika.
6 # 2 Kor 5:1 Hakika wema na fadhili zitanifuata
Siku zote za maisha yangu;
Nami nitakaa nyumbani mwa BWANA milele.

Iliyochaguliwa sasa

Zab 23: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia