Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 47

47
Utawala wa Mungu juu ya Mataifa
Kwa mwimbishaji. Ya Wakorahi. Zaburi.
1Enyi watu wote, pigeni makofi,
Mpigieni Mungu kelele kwa Sauti ya shangwe.
2 # Kum 7:21; Neh 1:5; Mal 1:14 Kwa kuwa BWANA Aliye juu, mwenye kuogofya,
Ndiye mfalme mkuu juu ya dunia yote.
3 # Zab 18:47 Atawatiisha watu wa nchi chini yetu,
Na mataifa chini ya miguu yetu.
4 # 1 Pet 1:4 Atatuchagulia urithi wetu,
Fahari ya Yakobo ambaye alimpenda.
5 # Zab 24:7-10; Mdo 1:9; Efe 4:8-10; 1 Tim 3:16 Mungu amepaa kwa kelele za shangwe,
BWANA kwa sauti ya baragumu.
6Mwimbieni Mungu, naam, imbeni;
Mwimbieni mfalme wetu, naam, imbeni.
7 # Zek 14:9; 1 Kor 14:15 Maana Mungu ndiye mfalme wa dunia yote,
Imbeni kwa akili.
8Mungu awamiliki mataifa,
Mungu ameketi katika kiti chake kitakatifu.
9Wakuu wa watu wamekusanyika,
Wawe watu wa Mungu wa Ibrahimu.
Maana ngao za dunia zina Mungu,
Ametukuka sana.

Iliyochaguliwa sasa

Zab 47: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia