6
Maono ya Nane: Magari Manne ya Vita
1Nikainua macho yangu tena, nikaona, na tazama, yanatokea magari ya vita manne, yanatoka kati ya milima miwili, na milima hiyo ilikuwa ni milima ya shaba. 2#Zek 1:8; Ufu 6:4,5Katika gari la kwanza walikuwa farasi wekundu; na katika gari la pili walikuwa farasi weusi; 3#Ufu 6:2na katika gari la tatu walikuwa farasi weupe; na katika gari la nne walikuwa farasi wa rangi ya kijivujivu. 4#Zek 5:10Nikajibu, nikamwuliza yule malaika aliyesema nami, Hawa ni nini, Bwana wangu? 5#Zab 68:17; Ebr 1:7,14; 1 Fal 22:19; Ayu 1:6; Dan 7:10; Lk 1:19; Ufu 7:1Malaika akajibu, akaniambia, Hawa ni pepo nne za mbinguni, zitokeazo baada ya kusimama mbele za Bwana wa dunia yote. 6#Yer 1:14Gari lile lenye farasi weusi latoka kwenda hata nchi ya kaskazini; nao farasi weupe wakatoka wakafuata nyuma yao; na wale wa rangi ya kijivujivu wakatoka kwenda hata nchi ya kusini. 7#Mwa 13:17Na wale wekundu wakatoka, wakataka kwenda huko na huko katika dunia; naye akawaambia, Haya! Tokeni, mwende huko na huko katika dunia. Basi wakaenda huko na huko katika dunia. 8#Mhu 10:4Ndipo akaniita, akaniambia akisema, Tazama, wale waendao mpaka nchi ya kaskazini wameituliza roho yangu katika nchi ya kaskazini.
Kutawazwa kwa Chipukizi
9Neno la BWANA likanijia, kusema, 10#Ezr 2:1Pokea vitu mikononi mwa baadhi ya watu waliohamishwa, yaani, Heldai, na Tobia, na Yedaya; na siku iyo hiyo enenda ukaingie katika nyumba ya Yosia, mwana wa Sefania, waliyoifikia kutoka Babeli; 11#Kut 28:36naam, pokea fedha na dhahabu, ukafanye taji, ukamvike kichwani Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu; 12#Isa 9:6; 4:2; Mik 5:5; Mal 3:1; Yer 23:5; 33:15; Zek 13:7; 3:8; Mk 15:39; Lk 1:78; Yn 1:45; Zab 80:15-17; Mt 16:18; Efe 2:20; Flp 2:9; Ebr 2:9ukamwambie, ukisema, BWANA wa majeshi asema hivi, ya kwamba, Tazama, mtu huyu ndiye ambaye jina lake ni Chipukizi; naye atakua katika mahali pake, naye atalijenga hekalu la BWANA. 13#Zab 21:5; 110:4; Isa 22:24; Ebr 3:1Naam, yeye atalijenga hekalu la BWANA; naye atauchukua huo utukufu; ataketi akimiliki katika kiti chake cha enzi; na kutakuwa na kuhani katika kiti chake cha enzi; na shauri la amani litakuwa kati ya hao wawili. 14#Mk 14:9Na hizo taji zitakuwa za Heldai, na Tobia, na Yedaya; na kwa fadhili za mwana wa Sefania; ziwe ukumbusho katika hekalu la BWANA. 15#Efe 2:13Nao walio mbali watakuja na kujenga katika hekalu la BWANA, nanyi mtajua ya kuwa BWANA wa majeshi amenituma kwenu. Na haya yatatokea, kama mkijitahidi kuitii sauti ya BWANA, Mungu wenu.