Matendo 8:29-31
Matendo 8:29-31 SRUVDC
Roho akamwambia Filipo, Sogea karibu na gari hili, ukaribiane nalo. Basi Filipo akaenda mbio, akamsikia anasoma kitabu cha nabii Isaya; akanena, Je! Yamekuelea haya unayosoma? Akasema, Nitawezaje kuelewa, mtu asiponiongoza? Akamsihi Filipo apande na kuketi pamoja naye.