Luka 21
21
Sadaka ya mjane
1 #
Mk 12:41-44
Akainua macho yake akawaona matajiri wakitia sadaka zao katika sanduku la hazina. 2Akamwona mjane mmoja maskini akitia mle senti mbili. 3#2 Kor 8:12 Akasema, Hakika nawaambia, huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote; 4maana, hao wote walitoa sadaka katika mali iliyowazidi, bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo.
Kuangamizwa kwa hekalu kwatabiriwa
5 #
Mt 24:1-21; Mk 13:1-19 Na watu kadhaa walipokuwa wakiongea habari za hekalu, jinsi lilivyopambwa kwa mawe mazuri na sadaka za watu, alisema, 6#Lk 19:44 Haya mnayoyatazama, siku zitakuja ambapo halitasalia jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomolewa.
Ishara na mateso
7Wakamwuliza wakisema, Mwalimu, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini ishara ya kuwa mambo hayo yako karibu kutukia? 8#Dan 7:22 Akasema, Angalieni, msije mkadanganyika, kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ndiye; tena, Majira yamekaribia. Basi msiwafuate hao. 9#Dan 2:28 Nanyi mtakaposikia habari za vita na fitina, msitishwe; maana, hayo hayana budi kutukia kwanza, lakini ule mwisho hauji upesi.
10 #
Isa 19:2; 2 Nya 15:6 Kisha aliwaambia, Taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; 11kutakuwa na mitetemeko mikubwa ya ardhi; na njaa na tauni mahali pengi; na mambo ya kutisha na ishara kuu kutoka mbinguni. 12#Lk 12:11 Lakini, kabla hayo yote hayajatokea, watawakamata na kuwaudhi; watawapeleka mbele ya masinagogi, na kuwaua magerezani, mkipelekwa mbele ya wafalme na watawala kwa ajili ya jina langu. 13Na hayo yatakuwa ushuhuda kwenu. 14#Lk 12:11-12 Basi, kusudieni mioyoni mwenu, kutofikiri-fikiri kwanza mtakavyojibu; #Mt 10:19 15#Mdo 6:10 kwa sababu mimi nitawapa kinywa na hekima ambayo watesi wenu wote hawataweza kushindana nayo wala kuipinga. 16Nanyi mtasalitiwa na wazazi wenu, na ndugu zenu, na jamaa zenu, na rafiki zenu, nao watawaua baadhi yenu. 17#Mt 10:21,22 Nanyi mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu. 18#Lk 12:7; 1 Sam 14:45 Lakini hautapotea hata unywele mmoja wa vichwa vyenu. 19#2 Nya 15:7; Ebr 10:36 Nanyi kwa subira yenu mtaziponya nafsi zenu.
Unabii wa kuangamizwa kwa Yerusalemu
20Lakini, hapo mtakapoona mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi, basi jueni ya kwamba uharibifu wake umekaribia. 21Ndipo walio katika Yudea na wakimbilie milimani, na walio katikati yake wakimbilie nje, na walio katika mashamba wasiuingie. 22#Hos 9:7; Kum 32:35; Yer 5:29 Kwa kuwa siku hizo ndizo za mapatilizo, ili yatimizwe yote yaliyoandikwa. 23#1 Kor 7:26 Ole wao wenye mimba na wanaonyonyesha katika siku hizo! Kwa kuwa kutakuwa na shida nyingi katika nchi, na hasira juu ya taifa hili. 24#Kum 28:64; Zek 12:3; Isa 63:18; Zab 79:1; Dan 8:10; Rum 11:25; Ufu 11:2 Wataanguka kwa ukali wa upanga, nao watatekwa nyara na kuchukuliwa katika mataifa yote; na Yerusalemu utakanyagwa na Mataifa, hadi majira ya Mataifa yatakapotimia.
Kuja kwa Mwana wa Adamu
25 #
Mt 24:29,30; Mk 13:24-26 Tena, kutakuwa na ishara katika jua, na mwezi, na nyota; na katika nchi dhiki ya mataifa wakishangaa kwa kuvuma kwa habari na mawimbi yake; #Isa 13:10; Eze 32:7; Yoe 2:31; Ufu 6:12-13; Zab 65:7 26#Isa 34:4 watu wakivunjika mioyo kwa hofu, na kwa kutazamia mambo yatakayoupata ulimwengu. Kwa kuwa nguvu za mbinguni zitatikisika. 27#Dan 7:13; Ufu 1:7; Mt 26:64 Hapo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika wingu pamoja na nguvu na utukufu mwingi. 28#Flp 4:4,5 Basi mambo hayo yaanzapo kutokea, changamkeni, mkaviinue vichwa vyenu, kwa kuwa ukombozi wenu umekaribia.
Funzo la mtini
29 #
Mt 24:32-35; Mk 13:28-31 Akawaambia mfano; Utazameni mtini na miti mingine yote. 30Wakati imalizapo kuchipuka, mwaona na kutambua wenyewe ya kwamba majira ya mavuno yamekwisha kuwa karibu. 31Nanyi kadhalika, mwonapo mambo hayo yanaanza kutokea, tambueni ya kwamba ufalme wa Mungu u karibu. 32Amin, nawaambieni, Kizazi hiki hakitapita kabla ya hayo yote kutimia. 33#Lk 16:17 Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
Mahimizo ya kuwa waangalifu
34 #
Lk 17:27; Mk 4:19; Mt 24:49 Basi, jihadharini, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafla, kama mtego unasavyo; 35#Isa 24:17; 1 The 5:3 kwa kuwa ndivyo itakavyowajia watu wote wakaao juu ya uso wa dunia nzima. 36#Mk 13:33; Ufu 6:17 Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu.
37 #
Lk 19:47; Yn 8:1 Basi, kila mchana alikuwa akifundisha hekaluni, na usiku huenda kulala katika mlima uitwao wa Mizeituni. 38Na watu wote walikuwa wakiamka mapema waende hekaluni ili kumsikiliza.
Iliyochaguliwa sasa
Luka 21: SRUVDC
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

: