Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Wakorintho 10

10
Maonyo kutoka historia ya Israeli
1 # Kut 13:21-22; 14:22-29 Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari; 2wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari; 3#Kut 16:4,35; Kum 8:3 wote wakala chakula kile kile cha roho; 4#Kut 17:6; Hes 20:11 wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo. 5#Hes 14:16,23,29-30 Lakini wengi sana katika wao, Mungu hakupendezwa nao; maana waliangamizwa jangwani. 6#Hes 11:4,34 Basi mambo hayo yalikuwa mifano kwetu, kusudi sisi tusiwe watu wa kutamani mabaya, kama wale nao walivyotamani. 7#Kut 32:6 Wala msiwe waabudu sanamu, kama wengine wao walivyokuwa; kama ilivyoandikwa, Watu waliketi kula na kunywa, kisha wakasimama wacheze. 8#Hes 25:1-18 Wala msifanye uasherati, kama wengine wao walivyofanya, wakaanguka siku moja watu elfu ishirini na tatu. 9#Hes 21:5-6 Wala tusimjaribu Bwana, kama wengine wao walivyomjaribu, wakauawa na nyoka. 10#Hes 16:41-49; 14:2,36; Ebr 3:11,17 Wala msinung'unike, kama wengine wao walivyonung'unika, wakauawa na mharibifu. 11#1 Pet 4:7 Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiwa na miisho ya nyakati.
12Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke. 13Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita muwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili muweze kustahimili.
14 # 1 Yoh 5:21 Kwa ajili ya hayo, wapenzi wangu, ikimbieni ibada ya sanamu. 15Nasema kama na watu wenye akili; lifikirini ninyi ninenalo. 16#Mt 26:26-28; Mk 14:22-24; Lk 22:19-20; Mdo 2:42 Kikombe kile cha baraka tukibarikicho, je! Si ushirika wa damu ya Kristo? Mkate ule tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo? 17#1 Kor 12:27; Rum 12:5 Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja; kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja. 18#Law 7:6,15 Waangalieni hao Waisraeli walivyokuwa kwa jinsi ya mwili; wale wazilao dhabihu, je! Hawana shirika na madhabahu? 19#1 Kor 8:4 Basi niseme nini? Ya kwamba kile kilichotolewa sadaka kwa sanamu ni kitu? Au ya kwamba sanamu ni kitu? 20#Kum 32:17; Law 17:7; Zab 106:37; Ufu 9:20 Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani. 21#2 Kor 6:15,16; Mal 1:7,12 Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani. 22#Kum 32:21 Au twamtia Bwana wivu? Je! Tuna nguvu zaidi ya yeye?
Fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu
23 # 1 Kor 6:12 Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vifaavyo. Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vijengavyo. 24#Rum 15:2 Mtu asitafute faida yake mwenyewe, bali ya mwenzake. 25#1 Kor 14:2-10,22 Kila kitu kiuzwacho sokoni kuleni, bila kuulizauliza, kwa ajili ya dhamiri; 26#Zab 24:1 maana, Dunia ni mali ya Bwana na vyote viijazavyo. 27#Lk 10:8 Na mtu asiyeamini akiwaalika, nanyi mnataka kwenda, kuleni kila kitu kiwekwacho mbele yenu bila kuulizauliza, kwa ajili ya dhamiri. 28#1 Kor 8:7 Lakini mtu akiwaambia, Kitu hiki kimetolewa kiwe sadaka, msile, kwa ajili yake yeye aliyewaambia, na kwa ajili ya dhamiri. 29Nasema, dhamiri, lakini si yako, bali ya yule mwingine. Maana kwa nini uhuru wangu uhukumiwe na dhamiri ya mtu mwingine? 30#1 Tim 4:4 Ikiwa mimi natumia sehemu yangu kwa shukrani, kwa nini nitukanwe, kwa ajili ya kitu nikishukuriacho? 31#Kol 3:17 Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lolote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu. 32#Rum 14:13 Msiwakoseshe Wayahudi wala Wagiriki wala kanisa la Mungu, 33#1 Kor 9:20-22 vile vile kama mimi niwapendezavyo watu wote katika mambo yote, nisitake faida yangu mwenyewe, ila faida yao walio wengi, wapate kuokolewa.

Iliyochaguliwa sasa

1 Wakorintho 10: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia