Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Wakorintho 12:1-8

1 Wakorintho 12:1-8 SRUV

Basi, ndugu zangu, kuhusu karama za roho, sitaki mkose kufahamu. Mwajua ya kuwa mlipokuwa watu wa Mataifa, mlichukuliwa kufuata sanamu zisizonena, kama mlivyoongozwa. Kwa hiyo nawaarifu, ya kwamba hakuna mtu anenaye katika Roho wa Mungu, kusema, Yesu amelaaniwa; wala hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu. Basi kuna karama tofauti; bali Roho ni yeye yule. Tena kuna huduma tofauti, na Bwana ni yeye yule. Kisha kuna uwezo tofauti wa kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote. Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana. Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule