1 Wakorintho 9:19-23
1 Wakorintho 9:19-23 SRUV
Maana, ingawa nimekuwa huru kwa watu wote, nilijifanya mtumwa wa wote, ili nipate watu wengi zaidi. Nilikuwa kama Myahudi kwa Wayahudi, ili niwapate Wayahudi; kwa wale walio chini ya sheria, nilikuwa kama chini ya sheria, (ingawa mimi mwenyewe siko chini ya sheria), ili niwapate walio chini ya sheria. Kwa wale wasio na sheria nilikuwa kama sina sheria, (si kwamba sina sheria mbele za Mungu, bali mwenye sheria mbele za Kristo), ili niwapate hao wasio na sheria. Kwa wanyonge nilikuwa mnyonge, ili niwapate wanyonge. Nimekuwa hali zote kwa watu wote, ili kwa njia zote nipate kuwaokoa watu. Nami nafanya mambo yote kwa ajili ya Injili ili kuishiriki pamoja na wengine.