1 Samweli 22
22
Daudi na wafuasi wake wakiwa Adalumu
1 #
Zab 57:1; 142:1; Yos 12:15; 2 Sam 23:13; 1 Fal 17:3; Mik 1:15; Ebr 11:38 Basi Daudi akaondoka huko, akakimbilia pango la Adulamu; na ndugu zake na watu wote wa ukoo wa baba yake waliposikia habari hiyo, wakamwendea huko. 2#Amu 11:3 Na kila mtu aliyekuwa katika hali ya dhiki, na kila mtu aliyekuwa na deni, na watu wote wenye uchungu mioyoni mwao, wakakusanyika kwake; naye akawa jemadari wao; nao waliokuwa pamoja naye walikuwa kama watu mia nne.
3 #
Mwa 47:11; Kut 20:12; Law 19:3; Kum 5:16; Mit 10:1; 23:24; Mt 19:19; Yn 19:25-27; Efe 6:2; 1 Tim 5:4 Kutoka huko Daudi akaenda Mispa ya Moabu; akamwambia mfalme wa Moabu, Tafadhali wakubalie baba yangu na mama yangu watoke huko waliko, wakakae kwenu, hata nitakapojua Mungu atakalotenda kwa ajili yangu. 4Akawaleta mbele ya mfalme wa Moabu, nao wakakaa pamoja naye wakati wote Daudi alipokuwa ngomeni. 5#2 Sam 24:11; 1 Nya 21:9; 2 Nya 29:25 Kisha nabii Gadi akamwambia Daudi, Usikae hapa ngomeni; ondoka, ukaende mpaka nchi ya Yuda. Ndipo Daudi akaondoka, akaenda zake, akakaa katika msitu wa Herethi.
Sauli awaua manabii huko Nobu
6Kisha Sauli akasikia ya kwamba Daudi ameonekana, na wale watu waliokuwa pamoja naye. Basi Sauli alikuwa akikaa Gibea, chini ya mkwaju katika mahali palipoinuka, naye alikuwa na mkuki wake mkononi, na watumishi wake wote wakimzunguka. 7#1 Sam 8:14 Naye Sauli akawaambia watumishi wake waliomzunguka, Sikieni sasa, enyi Wabenyamini; je! Huyu mwana wa Yese atawapa ninyi kila mmoja mashamba, na mashamba ya mizabibu, atawafanya kuwa wakuu wa watu maelfu, na wakuu wa watu mamia; 8#1 Sam 20:2; 18:3; 23:16-18 hata ninyi nyote mkanifitinia, wala hapana mtu anifunuliaye habari hii mwanangu afanyapo agano na mwana wa Yese, wala hapana mmoja wenu anayenisikitikia, wala kunifunulia ya kuwa mwanangu amemchochea mtumishi wangu, anivizie kama hivi leo?
9 #
1 Sam 21:1,7; 14:3 Ndipo akajibu Doegi, Mwedomi, aliyesimama karibu na watumishi wa Sauli, akasema, Mimi nilimwona mwana wa Yese akienda Nobu, kwa Ahimeleki, mwana wa Ahitubu. 10#Hes 27:21; 1 Sam 21:6,9 Naye akamwuliza BWANA kwa ajili yake, akampa vyakula, akampa na ule upanga wa Goliathi, Mfilisti. 11Ndipo mfalme akatuma watu waende kumwita Ahimeleki, kuhani, mwana wa Ahitubu, na jamaa yote ya baba yake, hao makuhani, waliokuwako huko Nobu; nao wakaenda kwa mfalme wote pia. 12Sauli akasema, Sikia sasa, Ewe mwana wa Ahitubu. Naye akaitika, Mimi hapa, bwana wangu. 13Sauli akamwuliza, Mbona mmefanya fitina juu yangu, wewe na mwana wa Yese? Kwa maana umempa mikate, na upanga, nawe umemwuliza Mungu kwa ajili yake, ili aniasi na kunivizia kama hivi leo? 14#1 Sam 19:4,5; 20:32; 24:11; Mit 31:9 Basi Ahimeleki akamjibu mfalme, akasema, Katika watumishi wako wote ni nani aliye mwaminifu kama Daudi, aliye mkwewe mfalme, tena msiri wako, mwenye heshima nyumbani mwako? 15Je! Mimi nimeanza leo tu kumwuliza Mungu kwa ajili yake? Hasha! Mfalme asinidhanie mimi, mtumishi wake neno hili, Wala jamaa yote ya baba yangu, kwa maana mimi, mtumishi wako siyajui hayo yote, yaliyopungua au yaliyozidi. 16Naye mfalme akasema, Kufa utakufa, Ahimeleki, wewe na jamaa yote ya baba yako.
17 #
Kut 1:17; Mdo 4:19; 5:29 Kisha mfalme akawaambia askari walinzi waliosimama karibu naye Geukeni, mkawaue hao makuhani wa BWANA, kwa sababu mkono wao u pamoja na Daudi, na kwa sababu walijua ya kuwa amekimbia, wasiniarifu. Lakini watumishi wa mfalme walikataa kunyosha mkono na kuwaangukia makuhani wa BWANA. 18#Zab 12:5; Mit 28:15; 1 Sam 2:31; Kut 28:40 Basi mfalme akamwambia Doegi, Geuka wewe, uwaangukie hao makuhani. Basi Doegi, Mwedomi, akageuka, akawaangukia makuhani, akaua siku ile watu themanini na watano wenye kuvaa naivera ya kitani. 19#Neh 11:32; Isa 10:32; Ayu 20:19,20; Zab 10:1-18; Isa 26:13 Kisha akaupiga Nobu, mji wa makuhani, kwa makali ya upanga, wanaume na wanawake, watoto na wanyonyao, na ng'ombe, na punda, na kondoo. 20#1 Sam 23:6; Amu 9:5; 1 Sam 2:33; Ayu 1:15,19 Na katika wana wa Ahimeleki, mwana wa Ahitubu, akaokoka mtu mmoja tu, aliyeitwa Abiathari, akamkimbilia Daudi. 21Naye Abiathari akamweleza Daudi ya kwamba Sauli amewaua makuhani wa BWANA. 22Daudi akamwambia Abiathari, Siku ile alipokuwako Doegi, Mwedomi, nilijua hakika ya kuwa atamwambia Sauli; mimi nimewapatia watu wote wa jamaa ya baba yako kifo. 23#1 Fal 2:26; Mt 24:9; Yn 15:20,21; 16:2; Ebr 12:1-3 Kaa wewe pamoja nami, usiogope; kwa maana yeye atafutaye roho yangu, ndiye atafutaye na roho yako; nawe utakaa kwangu salama.
Iliyochaguliwa sasa
1 Samweli 22: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

: