1 Timotheo 6
6
1 #
Efe 6:5; Tit 2:9,10 Wote walio chini ya nira ya utumwa, wawachukulie bwana zao kama wanaostahili heshima yote, ili jina la Mungu na mafundisho yetu yasitukanwe. 2#Flm 1:16 Na wale walio na bwana waaminio wasiwadharau kwa kuwa ni ndugu; bali afadhali wawatumikie, kwa sababu hao wapatao faida ya kazi yao wamekuwa wenye imani na kupendwa.
Mafundisho ya uongo na utajiri halisi
Mambo hayo uyafundishe na kuyahimiza.
3 #
Gal 1:6-9; 2 Tim 1:13 Mtu awaye yote akitoa mafundisho mengine, wala hayakubali maneno yenye uzima ya Bwana wetu Yesu Kristo, wala mafundisho yapatanayo na utauwa, 4amejivuna; wala hafahamu neno lolote; bali ana wazimu wa kuwazia habari za maswali, na mashindano ya maneno, ambayo katika hayo hutoka husuda, na ugomvi, na matusi, na shuku mbaya; 5#2 Tim 3:8; 4:4; Tit 1:14 na kuzozana miongoni mwa watu waliopotoka katika akili zao, walioikosa kweli, huku wakidhani ya kuwa utauwa ni njia ya kupata faida. 6#1 Tim 4:8; Ebr 13:5; Flp 4:11,12 Lakini utauwa pamoja na kuridhika ni faida kubwa. 7#Mhu 5:14; Ayu 1:21 Kwa maana hatukuja na kitu duniani, tena hatuwezi kutoka na kitu; 8#Mit 30:8 ila tukiwa na chakula na nguo tutaridhika na vitu hivyo. 9#Mit 23:4; 28:22 Lakini hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu na mtego, na tamaa nyingi zisizo na maana, zenye kudhuru, zinazowaingiza watu katika upotevu na uharibifu. 10#Efe 5:5 Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi.
Vita vizuri vya imani
11 #
2 Tim 2:22
Bali wewe, mtu wa Mungu, uyakimbie mambo hayo; ukafuate haki, utauwa, imani, upendo, subira, upole. 12#1 Kor 9:25,26; 2 Tim 4:7 Piga vita vile vizuri vya imani; shika uzima ule wa milele ulioitiwa, ukaungama maungamo mazuri mbele ya mashahidi wengi. 13#Yn 18:36,37; 19:11 Nakuagiza mbele za Mungu anayevihifadhi hai vitu vyote, na mbele za Kristo Yesu, aliyeyaungama maungamo mazuri yale mbele ya Pontio Pilato, 14kwamba uilinde amri hii pasipo mawaa, pasipo lawama, hata kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo; 15#1 Tim 1:11; Ufu 17:14; Kum 10:17 ambako yeye kwa majira yake atakudhihirisha, yeye aliyehimidiwa, Mwenye uweza peke yake, Mfalme wa wafalme, Bwana wa mabwana; 16#Kut 33:20 ambaye yeye peke yake hapatikani na mauti, amekaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa; wala hakuna mwanadamu aliyewahi kumwona, wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye hata milele. Amina.
17 #
Zab 62:10; Lk 12:20; Rum 12:16 Walio matajiri wa ulimwengu wa sasa uwaagize wasijivune, wala wasiutumainie utajiri usio yakini, bali wamtumaini Mungu atupaye vitu vyote kwa wingi ili tuvitumie kwa furaha. 18Waamuru watende mema, wawe matajiri katika kutenda mema, wawe wakarimu na wawe tayari kushiriki na wengine; 19#Mt 6:20 huku wakijiwekea akiba iwe msingi mzuri kwa wakati ujao, ili wapate uzima ulio kweli kweli.
Maagizo kwa Timotheo na baraka
20 #
1 Tim 4:7; 2 Tim 1:14 Ee Timotheo, ilinde hiyo amana; ujiepushe na mazungumzo yasiyo ya kimungu, yasiyo na maana, na mashindano ya elimu iitwayo elimu kwa uongo; 21#1 Tim 1:6; 2 Tim 2:18 ambayo wengine kwa kuikiri wamepoteza Imani. Neema na iwe pamoja nanyi.
Iliyochaguliwa sasa
1 Timotheo 6: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

: